Mwakilishi kutoka taasisi ya Zara Charity Bw. Datuc Joseph (katikati) akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Meneja wa kampuni ya Tigo, Bw. William Mpinga.
**********
Tigo Tanzania kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya Kiserikali ya ZARA Charity, taasisi tanzu ya kujitolea ya kampuni ya Utalii ya ZARA Tanzania Adventures ambayo husaidia shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujitolea leo imezindua Mbio za Sita za Nusu marathon (kilomita 21.1) zijulikanazo kama ‘Ngorongoro Half Marathon’ zinazotarajiwa kufanyika jumamosi ya Aprili 6, mwaka 2013.
Mashindano hayo ya mbio kwa mwaka huu yamebeba ujumbe wa ‘Mbio za Mapambano dhidi ya Malaria’ yatafanyika katika mji mdogo wa Karatu mkoani Arusha.
Mnamo mwaka 2010, kampuni ya Zara Tanzania adventures ilianzisha na kuwa mdhamini mkuu wa mbio za watoto za kilomita tano zilipewa jina la ‘Ngorongoro Run: Kids’ Fun Run’, mbio ambazo zimetia chachu zaidi mbio hizo za Ngorongoro Marathon.
Zaidi ya wakazi 5,000 wa Karatu wanashiriki na kuzifurahia sana mbio hizo ambapo pia hupata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya mapambano dhidi ya malaria.
Mbio za Ngorongoro Marathon mwaka huu ni za kipekee sana kwani zinajumuisha ushindanishaji wa makampuni mbalimbali ulioandaliwa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Tigo yatakayofanyika kabla ya kuanza kwa mashindano hayo ambapo mshindi ataibuka na kitita cha dola za kimarekani 20,000 ambazo atajitolea kwa taasisi yeyote yenye uhitaji atakayoichagua.
Pia, Tigo wameandaa shindano kwa vyombo vya habari ambapo wanahabari watashindanishwa kujishindia safari ya kwenda Karatu mkoani Arusha kushiriki mbio hizo, ambapo washindi watadhaminiwa safari hiyo na Tgo.
Ufunguzi wa mbio hizo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 3000 ambapo Mgeni Rasmi atakayefungua mbio hizo anatarajiwa kuwa Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.
“Tigo inayo furaha kubwa sana kushirikishwa katika kuandaa mbio za Ngorongoro Marathon ikiwa na jukumu kubwa la kuwaelimisha wananchi namna ya kupambana na malaria , ugonjwa ambao unapoteza mamilioni ya Watanzania kila mwaka. Tangu mwaka 2009, kampnuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kuasidia shughuli mbalimbali za masuala ya Afya kwa watanzania kupitia shughuli mbalimbali na tunajivuinia kupambana na malaria kupipitia mbio hizi. Mahusiano yetu na Zara Tours katika kudhamini mbio hizi yamekuwa ya muhimu na ya mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwa mbio hizi mwaka 2008, hasa ikizingatiwa kuwa afya kwanza.” Alifafanua William Mpinga, Menja Chapa wa Tigo.
Mwakilishi kutoka taasisi ya Zara Charity Bw. Datuc Joseph, alisema, “Zara Charity ilianzisha mbio za Ngorongoro Marathon, kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii kupambana na malaria, kuboresha huduma za hosptali pamoja na huduma ya mama na motto. Lengo letu kuu ni kutoa elimu ya mapambano dhidi ya malaria, kutoa suluhisho kwa wadau mbalimbali njia mbadala za kuwezesha upatikanaji wa huduma za malaria hasa katika maeneo ambayo yamekumbwa zaidi na ugonjwa huo. Tunatambua mchango mkubwa sana ambao umefanywa na kampuni ya Tigo katika suala hili na ninaamini kuwa utawasaidia watanzania wengi”
Post a Comment