Mshereheshaji wa Umoja wa Serekali za Wanafunzi Zanzibar Hissham Muamed Abdukadir akisoma ratiba ya Kongamano linalouliza sababu zinazopelekea kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa Zanzibar.
Msanii Ali Husen (wakulia) kutoka USEWAZA akimshawishi wanafunzi Abdallah Juma katika igizo kutumia madawa ya kulevya jambo ambalo halikubaliki katika Ukumbi wa Cafe Restaurant Bwawani Mjini Zanzibar.
Katibu wa USEWAZA Salum Humoud Salum akinukuu badhi ya sababu zilizopelekea kushuka kwa ufaulu kwa wanafunzi wa Zanzibar zilizoandikwa kwenye gazeti la Zanzibar Leo.katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Cafe Restaurant Bwawani Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu Zanzibar wa pili (kushoto) Sleman Yahya Ame akijibu maswali alioulizwa na walim na wanafunzi waliofika kwenye Kongamano hilo,wakwanza (kulia) Haji Kutenga Mlezi USEWAZA,anaefata Abdulla Bakari Khamis Mahusiano (WEMA) na wakwaza kushoto,Sleman Takadir.
Mwanafunzi Monika Samuel Makoya kutoka Skuli ya Kinuni akiuliza swali juu ya uhaba wa vifaa vya sayansi na walimu wake kwa Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu Zanzibar Huko katika Ukumbi wa Cafe Restaurant Bwawani Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).