Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

'NJIANI KWENDA KWA RAIS' - 3


1 6eab2

Ndugu zangu,
Jana nilimalizia kwa kuandika haya; “miezi michache tu baada ya tukio lile Ubalozini, marafiki wawili; Julius na Oscar walifunga safari ya kwenda China. Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kwenda China.

Huko China Julius na Oscar waliiona China kwa ‘ miwani tofauti’. Ni nini kilitokea kwa marafiki wawili hawa, Oscar na Julius, waliporudi nyumbani?” – Endelea na simulizi hii.

Ndugu zangu,
Hakika, sikufikiri kuwa simulizi hii ingewavutia wengi hivi. Nami nimehamasika kusimulia zaidi. Na hapa ieleweke, kuwa ninapomsoma Mwandishi Stig Holmqvist nalinganisha pia anachokiandika na yale yaliyopatwa kuandikwa na kusimuliwa na wengine. Yale ambayo hata mimi utotoni nimepata kusimuliwa na hata kuyaona. Hivyo, nafanya uchambuzi wa jumla. Msije basi mkashangaa nitakapowarejea waandishi wengine hata yale ambayo mimi mwenyewe nimepata kuyaandika huko nyuma.
Mathalan, wale waliotaka kujua kama kitabu cha Holmqvist kinapatikana kwa lugha ya Kiingereza, jibu lake ni hapana. Lakini, mengine anayosimulia Holmqvist unaweza pia kuyapata kwa lugha ya Kiingereza kwenye vitabu vya waandishi kama ( The Critical Phase in Tanzania 1945-68:Nyerere and the Emergence of a Socialist Society, Cranford Pratt ) , ( Nyerere of Tanzania, William Edgett Smith) na hata( The Dark Side Of Nyerere’s Legacy, Ludovick Mwijage) Hiki kimepigwa marufuku.
(Ninanavyo vitabu hivyo na vinginevyo kwenye maktaba yangu kwa anayetaka kuniazima)
Tuje basi kwenye mwendelezo wa simulizi hii;
Kama inavyoonekana kwenye maandiko ya Stig Holmqvist, kuwa Oscar na Julius waliiona China kwa miwani tofauti.
Julius aliona nini China?

Julius alivyutiwa sana Kiongozi Mkuu Mao. Aliona kuna mengi yanayofanana kati ya China na Tanzania.
Vile Mao alivyowakusanya Wachina kwenye vijiji ilirahisisha kuwafikishia ujumbe kwenye mapambano dhidi ya njaa, umasikini na maradhi. Kwamba ndio njia nzuri ya kuifanya nchi kujitegemea kwa watu wake kushiriki kazi za uzalishazji kijamaa. Lakini pia, kuondokana na sauti zenye kupinga; hivyo kuondokana na upinzani.
Ya China yalifanana sana na fikra za Julius. Na akikumbuka mkutano ule mgumu na Balozi wa Marekani pale Dar, Julius alianza kuiona njia ya kuachana kabisa na Wamarekani. Pamoja na kumwagiwa sifa na John Kennedy alipotembelea White House kwa mara ya kwanza. Julius aliuona ugumu wa kufanya kazi na Wamarekani.
Oscar aliona nini China?
Oscar hakuvutiwa kabisa na Mao. Hakuamini kuwa njia ya Mao ni sahihi pia kufuatwa na Tanzania. Kwenye moja ya kumbukumbu ya ziara yao ya China, kumbukumbu ambazo Oscar hakupata kuzichapisha, anasema; “ Mao anafanywa kama Mungu. Kutukuzwa kwa Mao hakukumshtua Nyerere, hakuna alichohoji. Mao anakuwa mfano wa kuigwa kwa Nyerere. Na Nyerere anabadili hata staili ya mavazi yake.” ( Oscar Kambona, Pa vag till presidenten, ukurasa wa 200)
Oscar alikubaliana na Julius kuwa Chama kimoja kinaweza kuwa mkakati mzuri kuzuia mgawanyiko wa kikabila na kimaslahi kama inavyotokea mara nyingi katika nchi za Afrika, na hilo la mwisho walikubaliana lisitokee.
Mara baada ya kurudi kutoka China, haikupita muda, Tanzania ikafanywa kuwa nchi ya Chama kimoja.
Hata hivyo, Oscar na Julius hawakukubaliana juu ya kwa namna gani mamlaka ya uongozi yangegawanywa ndani ya Chama. Na kwa namna gani demokrasia ya mazungungumzo ingeendelezwa ndani ya Chama.
Tangu hapo, dalili za marafiki wawili kuanza kufarakana zikaanza kudhihiri. Na hiki hasa kikawa ni kisa cha marafiki watatu ambacho nilipata kukisimulia kwenye makala zangu za kwenye Raia Mwema. Na marafiki watatu hapa ni Kambarage ( Julius) Kawawa( Rashid) na Kambona ( Oscar). Na ajabu ya marafiki hawa, wote watatu wana majina ya pili yenye kuanzia na herufi ‘ K’.
Ndio, wote hawa walikuwa ni viongozi vijana kwenye nchi changa. Walikuwa pia na ushawishi kwenye jamii.
Na ili tufahamu zaidi urafiki wa watatu hawa ni vema tufahamu jinsi walivyokutana;
Nyerere alikutana na Oscar Kambona wakati Kambona alipokuwa shuleni Tabora mwishoni mwa miaka ya 40. Inasemwa, kuwa Nyerere alimtangulia kiumri Oscar kwa kupishana miaka mitatu tu. Kule Tabora Nyerere alikutana pia na Rashid Kawawa, naye alimzidi kiumri kwa miaka mitatu hivi.
Hivyo basi, twaweza kusema, kuwa urafiki wa Julius, Oscar na Rashid ulianzia Tabora, na harakati zao za pamoja za mapambano ya kisiasa zilianzia huko huko Tabora.
Ni nini basi kilifuatia kwenye urafiki wao ? Simulizi hii itaendelea...
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top