Hatimaye makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba
Godfrey Nyange Kaburu ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake kwenye klabu ya
Simba mapema leo.
Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi wa Simba ambazo
mtandao huu umezipata ni kwamba Kaburu leo ametuma barua pepe kwenda kwa
mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh.Aden Rage akimuelezea maamuzi yake ya kujivua
madaraka ya kuitumikia Simba kutokana mgawanyiko mkubwa uliopo kwenye uongozi wa
klabu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari Kaburu ameelezea kwamba
kamati ya utendaji imegawanyika na ufa uliopo hautoi nafasi nzuri kwake
kuitumikia vizuri Simba, akisema ni moja ya sababu ya timu yao ya Simba
kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali inayoshiriki.
Pia Kaburu
amesema amechukua maamuzi hayo ni njia mojawapo ya kuwajibika kama kiongozi
kutokana mambo kutokwenda vizuri hali ambayo imesabababisha kutukanwa na
kupigiwa kelele nyingi na wanachama na wapenzi wa Simba SC Mwenyekiti. Hivyo
ameamua kujiuzulu kupisha wanachama wengine wa Simba waweze kuliongoza jahazi la
klabu hiyo.
Katika
hatua nyingine mwenyekti wa kamati ya usajili na mjumbe ya kamati ya utendaji
Zacharia Hans Pope nae ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi zote alizokuwa
akishikilia Simba.
Pia kwenye taarifa yake ya kujiuzulu Pope
amesema mgawanyiko uliopo kwenye uongozi ndio chanzo cha kujiuzulu kwake katika
kuitumikia Simba kupitia nafasi za uongozi alizokuwa nazo kwa takribani miaka
3.
Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi wa Simba ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Kaburu leo ametuma barua pepe kwenda kwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh.Aden Rage akimuelezea maamuzi yake ya kujivua madaraka ya kuitumikia Simba kutokana mgawanyiko mkubwa uliopo kwenye uongozi wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari Kaburu ameelezea kwamba kamati ya utendaji imegawanyika na ufa uliopo hautoi nafasi nzuri kwake kuitumikia vizuri Simba, akisema ni moja ya sababu ya timu yao ya Simba kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali inayoshiriki.
Pia Kaburu amesema amechukua maamuzi hayo ni njia mojawapo ya kuwajibika kama kiongozi kutokana mambo kutokwenda vizuri hali ambayo imesabababisha kutukanwa na kupigiwa kelele nyingi na wanachama na wapenzi wa Simba SC Mwenyekiti. Hivyo ameamua kujiuzulu kupisha wanachama wengine wa Simba waweze kuliongoza jahazi la klabu hiyo.
Katika
hatua nyingine mwenyekti wa kamati ya usajili na mjumbe ya kamati ya utendaji
Zacharia Hans Pope nae ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi zote alizokuwa
akishikilia Simba.
Pia kwenye taarifa yake ya kujiuzulu Pope
amesema mgawanyiko uliopo kwenye uongozi ndio chanzo cha kujiuzulu kwake katika
kuitumikia Simba kupitia nafasi za uongozi alizokuwa nazo kwa takribani miaka
3.
Post a Comment