Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe
kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya
Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert
Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert
Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete
kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini
wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu
Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika
sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo
Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za
miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es
salaam, leo Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakiangalia watoto wachanga
waliotunzwa katika chumba maalum muda
mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu
mbalimbali za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa
mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi
16, 2013.
Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka
25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi
16, 2013
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria sherehe za miaka 25
ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16,
2013
Sehemu ya wageni waalikwa na wanafunzi na wafanyakazi wa
hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25
ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16,
2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri
Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert
Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013. Picha na IKULU
*********
*********
RAIS Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuwasogezea karibu huduma za afya wananchi popote walipo nchini.
Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya utoaji huduma za afya, katika hospitali ya Hubert Kairuki.
Alisema serikali imejipanga vizuri katika kuzijengea uwezo hospitali kwa kuongeza madaktari, ili kuondokana na changamoto zinazowakabili kwa kuwahudumia wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.
Kikwete alisema mipango wa ujenzi wa Chuo cha Mlogazila imekamilika, ambacho kinatarajiwa kuzalisha wataalamu 12,000 kwa mwaka kitakapoanza.
“Kuna watu kazi yao ni kukebehi kila kinachofanywa wakidhani kuwa kama wangekuwa wao wangeweza kufanya kirahisi, bila kujua kila kinachofanyika kina mchakato wake hata hivyo, sisi tutafanya”alisema Kikwete.
Kikwete alisema hivi sasa serikali inakusudia kuziimarisha hospitali zote hapa nchini ili kuondokana na tabia ya kuwasafirisha wagonjwa kwenda nje kwa ajili ya baadhi ya matibabu.
Aidha, aliupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kutokana na juhudi zake za kutoa huduma hiyo ya miaka 25 bila kutetereka ambapo pia imeanzisha kituo cha kupambana na kuzuia vifo vya watoto pamoja na akina mama wajawazito.
Vilevile alizitaka hospitali hizo za binafsi kujitahidi kuboresha huduma zake hadi zilingane na huduma zinazotolewa katika nchi za nje kama vile India.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Asser Mchomvu alisema tangu kuanzishwa kwake iliweza kuhudumia wagonjwa milioni tatu.
Alisema mafanikio hayo yalitokana na ushirikiano uliyojengeka kati ya wafanyakazi wa hospitali hiyo, kuanzia ngazi ya chini hadi juu.
Post a Comment