Rais Jakaya Kikwete,
Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri
Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili
wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani
Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi
ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada
ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa
Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Rais Jakaya Kikwete,
akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo
la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika
Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika
Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa
shinikizo la damu
Rais Jakaya Kikwete,
Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa
Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed
Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha
CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Waombolezaji wakibeba
jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa
safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. Picha na
OMR
Post a Comment