Shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais nchini Kenya,
ilisimamishwa usiku kucha kwa sababu ya hitilafu za mitambo ya tume huru ya
uchaguzi na mipaka iliyokuwa inatumika kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa
Kenya.
Maafisa wa tume hiyo, wamelazimika kusafiri kwa barabara kutoka umbali wa
maelfu ya kilomita ili kwenda katika kituo cha kutangazia matokeo ya kura za
urais mjini Nairobi kuwasilisha fumo zao za matokeo.Maafisa wa uchaguzi wametoa wito wa utulivu na amani kwa wakenya wakati tume ikiendelea kutatua tatizo la kura.
Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta,ambaye anatakikana na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya, miaka mitano iliyopita, angalia yuko mbele katika matokeo ya uchaguzi wa urais.
Post a Comment