Kampeni Kabambe ya
kuitangaza Bia ya Serengeti Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti
(SBL) ijulikanayo kama TUPO PAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO imelitikisa mitaa
na vitongoji vya jiji la Dar es Salaam jana.
Huku pakiwa na burudani ya
muziki ambayo iliashiria Shangwe za mafanikio, Msafara wa magari kadhaa ya
Kampuni ya Bia ya SBL pamoja na Lori kubwa aina ya Scania Semitrailer likiwa
limepambwa vilivyo na kuleta mvuto wa ajabu kwa Watanzania lilikatika mitaa
mbalimbali ya jiji.
Msafara huo wa kutoa
Shukrani kwa Watanzania ndani ya jiji la Dar es Salaam ulianzia katika Kiwanda
cha SBL Temeke kisha kwenda hadi Mwembeyanga hadi Saba
saba.
Shangwe hizo ziliendelea
hadi Taifa, Chang'ombe, Kamata, Msimbazi, kisha msafara huo ukaingia baranbara
ya uhuru, ukapita Ilala ukaja tokea Buguruni, ukaingia Barabara ya Mandela hadi
Ubongo kisha ukapita Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, ukaelekea Sinza ukatokea
Bamaga ukafuata barabara ya Bagamoyo hadi Victoria ukaingia Mwananyamala na
kumalizia viwanja vya Biafra Kinondoni.
Aidha shsngwe hizo zilikuwa
zikiendelea katika maeneo kadhaa ya sehemu za starehe za Miti Mirefu, Kimara,
Jambo park jet Lumo, Huduma Mbagala na Airtel Pub Banana.
Ni mwendo wa Shangwe tu
ulikuwa ukiemdxelea kila kona Gari hilo lilipopita. Mbali na kampeni hii katika
Mitaa ambayo imeanzia jijini Dar es Salaam na pia itasambaa mikoani pia
Matangazo katikia vituo vya televisheni, Redio, Magazeti na Blogs yatakuwa
yanatoka pamoja na mitaani.
Magari mengine yalikuwa
Nyuma na kupambwa na chapa mbalimbali za Bidhaa za kampuni ya
SBL.
Tupo Pamoja katika Shangwe
za Mafanikio...
SOURCE FATHER KIDEVU
Post a Comment