Kijana Mafuvu akionyesha umahili
wake wa kucheza katika Shindano la Moro Carnival ambalo lilikuwa
likiwapambanisha vijana wa mji wa Morogoro kuonyesha vipaji vyao mbali
mbali. Shindano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sabasaba mjini
Morogoro, Moro Carnival lengo lake ni kuvumbua vipaji wa kuwashindanisha
na kuviendeleza vipaji kwa vijana wa mji wa Morogoro. Vipaji
vilivyokuwa vikitafutwa ni vya kudansi, kuimba, wasanii wa muziki wa Hip
Hop, Uchekeshaji n.k.
Watu waliojitokeza katika shindano hilo wakifuatatilia kwa makini mchuano.
Majaji wa Shindano la Moro
Carnival lililofanyika katika uwanja wa sabasaba, kutoka kulia ni Frado
John, Msanii wa Muziki wa bongofleva Seleman Msindi 'Afande Sele',
Wiliam Matajiri pamoja na mwanadada Adela Tilya.
Jaji nambali moja Frado John akitoa makisi kwa mshiriki wa shindano la Moro Carnival.
Jaji nambali mbili Seleman Msindi 'Afande Sele' akitoa makisi kwa mshiriki.
Mshiriki wa muziki wa hip hop,
akionyesha makali yake ya kuchana wakati wa shindano la Shindano la Moro
Carnival lililofanyika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.
Post a Comment