Washiriki
wa Miss Utalii tanzania wakiwa katika moja ya Makaburi ya zamani Kaole
Bagamoyo.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012-13
wakiwa katika mazoezi ya Nguvu ndani ya ukumbi wa Dar Live.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012-13
wakiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Mtwana Catering Service ambaye ndiye
anaye walisha Warembo hao.
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania 201213 wakitoa Burudani ya Nguvu katika Jukwaa la Sanaa
(BASATA).
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania wakiwa Katika Picha ya Pamoja Baada ya kumaliza Mazoezi
yao Katika Ukumbi wa Dar Live.
--
Wakati maandalizi ya Fainali za
Taifa za kumpata Miss Utalii Tanzania 2012/13 yakiwa yanaendelea kwa kasi kubwa,
Bodi ya Utalii Tanzania itaendesha Semina Maalum ya Mafunzo ya Utalii kwa
washiriki wote walioko kambini Ikondolo Lodge Kibamba wakijiandaa na Fainali za
Taifa zitakazo fanyika Mwishoni mwa wiki ijayo Jijini Dae es
salaam.
Akithibitisha taarifa hizo kwa
waandishi wa Habari Raisi wa Kamati ya Mashindano hayo Erasto G. Chipungahelo
alisema kuwa Semina hiyo maalum itakayo endeshwa na Bodi yaUtalii Tanzania
itafanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Utalii uliyopo katika ofisi za Bodi ya
Utalii jingo la IPS Dar es salaamsiku ya Alhamisi Tarehe 7.03.2013 kuanzia saa
Tatu asubuhi na kuwashirikisha zaidi ya Warembo 40 wakiwakirisha Mikoa yote ya
Tanzania Bara , Kanda maalum za Vyuo vikuu na Zanzibar. Watoa mada wakuu katika
semina hiyo, itakuwa ni wataalam walio bobea katika secta ya utalii na masoko ya
utalii kutoka Bodi ya Taifa ya Utalii(Tanzania Tourist Board).
Kwa niaba na kamati ya Miss
Utalii Tanzania, Ninatoa shukurani za pekee kwa Serikali na Bodi nzima ya Utalii
kwa kuendesha semina hii muhimu kwa washiriki wa Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania ambapo washindi wa kwanza mpaka wa Tano watawakirisha Tanzania katika
mashindano mbalimbali ya utalii ya Dunia. Yakiwemo ya Miss Tourism World,
International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation World , Miss
Tourism university World na Miss Heritage World. Yatakayo fanyika katika nchi
mbalimbali kuanzia mwezi wa nne mwaka huu.
Hii ni fulsa ya pekee kwa
washiriki na washindi watakao patikana katika fainali za Taifa kuweza kujua na
kujifunza juu ya utalii Tanzania, mbinu na mikakati ya kutangaza vivutio vya
kitalii kitaifa na kimataifa, hivyo kutusaidia kutimiza ndoto na malengo yetu ya
miaka mitano ya kutwaa Mataji matatu ya Dunia mwaka 2013.
Maandalizi katika kambi ya
warembo yanaendelea vizuri , ushindani ni mkubwa ari na dhamira ya kila Mrembo
kulinda hadhi na Heshima ya Mkoa wake kwa kutwaa taji la Taifa ni
kubwa.
Chipungahelo aliongeza kwamba,
ili kuthibitisha hayo, anaomba watanzania wote wakazi wz Dar es salaam na Mikoa
ya Jirani, wajitokeze kwa wingi siku ya ya Jumamosi Tar 9.03.2013 usiku katika
ukumbi wa Dar Live Mbagala kushuhudia warembo hawa wakipanda jukwaani kuwania
Tuzo mbalimbali za Vipaji na Utamaduni. Ambapo mbali na kupita jukwaani na
mavazi mbalimbali washiriki wote pia watashindana kucheza na kuimba nyimbo za
Asili za Mikoa wanayo wakilisha. Na hili litakuwa ni tukio la kihistoria la
Utalii, Urembo na Utamaduni kuwahi kufanyika hapa Tanzania kabla na Baada ya
Uhuru.
Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge,
Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers,
TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey
Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa
(BASATA ) www.misstourismorganisation. blogspot.com
Erasto G.
Chipungahelo
Raisi Miss Utalii
Tanzania
Post a Comment