Mrisho ngasa wa timu ya
Simba akijaribu kumtoka beki wa Libolo ya Angola katika mechi ya kwanza
iliyochezwa jijini Dar es Salaam.
SIMBA leo wanakabiliwa
na mtihani wa kufanya maajabu mengine katika historia ya soka Tanzania wakati
watakapowavaa Recreativo Libolo ya Angola ugenini, huku Azam FC wakishuka
dimbani kulinda ushindi wao wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Al Nasri ya Sudan
Kusini.
Pambano la Azam
linafanyika kwenye mji wa Juba, ambapo wanahitahi sare aina yoyote ili kusonga
mbele raundi ya pili
Katika pambano la
Simbalitakalochezwa saa tisa za Angola ikiwa ni saa 11 kwa saa za Afrika
Mashariki na kati, Simba wataingia katika uwanja wa Calulukuumana na Libolo
wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 wiki mbili zilizopita muuaji akiwa Joao
Martins.
Katika pambano la leo,
kocha Patrick Liewing huenda akamkosa kiungo mahiri, Mwinyi Kazimoto ambaye
tangu awasili nchini Angola amekuwa akisumbuliwa na jino.
Nafasi yake inatazamiwa
kuchezwa na kinda, Abdallaa Seseme ambaye alikuwa nyota wa mchezo katika pambano
la Ligi kuu dhidi ya Prisons wiki moja iliyopita. Kama Kazimoto akipata nafuu
kabla ya mechi basi huenda Seseme akaanzia benchi.
Kocha Liewig ambaye ni
raia wa Ufaransa amepanga kucheza soka la kushambulia na kutengeneza nafasi kwa
ajili ya kurudisha bao la Martins ambalo limeiweka Simba katika nafasi mbaya ya
kusonga mbele.
Tutajaribu kufunga mabao
ya mapema kwa ajili ya kurudisha bao lao.
Najua wachezaji wangu
wanaweza kufanya hivyo kwa sababu katika mechi ya kwanza tulitengeneza nafasi
nyingi lakini hatukutumia, wao walitengeneza chache na walitumia,î alisema
Liewing.
Liewig pia aliongeza
kuwa kutokana na wachezaji wengi wa Libolo kuwa na nguvu, stamina atawataka
wachezaji wake wajaribu kukaa na mpira kwa muda mwingi wakiepuka matumizi ya
nguvu ya Libolo.
Pambano hilo
linatazamiwa kuchezeshwa na Mwamuzi wa kati, Nhleko Simanga kutoka Swaziland ,
waamuzi wasaidizi ni Nkhabela Bhekisizwe na Mbingo Petros pamoja na mwamuzi
msaidizi Fabuze Mbongiseni wote kutoka kutoka Swaziland pia. Kamisaa wa pambano
hilo ni Mandla Mazibuko kutoka Afrika Kusini.
Mwamuzi Simanga anaweza
kuwa na bahati nyingine kwa Simba leo kwa sababu ndiye aliyechezesha mechi kati
ya Simba na Shandy ya Sudan, ambapo Simba walishinda 3-0 kwa mabao ya Emmanuel
Okwi, Haruna Moshi na Patrick Mutesa Mafisango ambaye kwa sasa ni
marehemu.
Endapo Simba itashinda
leo itakuwa imerudia historia ya mwaka 1979 ambapo ilifungwa 4-0 nyumbani na
Mufulira Wanderers, lakini ikashinda 5-0 ugenini jijini
Lusaka.
Katika pambano la leo,
Simba ambayo imefikia katika Hotel ya Ritz inayomilikiwa na tajiri wa Libolo,
Lui Compos inatazamiwa kuwakilishwa na Juma Kaseja, Said Nassor Chollo, Amir
Maftah, Juma Nyosso, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Haruna Chanongo, Amri
Kiemba, Abdala Seseme, Felix Sunzu, Mrisho
Ngassa.
Post a Comment