UNIVERSITY OF DAR ES
SALAAM
Academic Staff
Assembly
Utangulizi
Wapendwa waandishi wa
habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali
ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa
uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi
tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna
baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea
wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua
nchini.
Migogoro hii ilianza
kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia
uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule
Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi
viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako
tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.
Mbali na hayo, kuna
matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha migogoro ya kidini
kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia yakitokea sekondari za Bagamoyo,
Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko. Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu
udini kwenye sehemu za kazi na kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo
wanaodai kuwa baadhi ya taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali
zinazohudumia watanzania wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya
kupendelea dini fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni
vema likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na kusababisha
watanzania wasielewane.
Post a Comment