Wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakigonganisha glasi za mvinyo wa matunda ya Mananasi
uliotengenezwa nchini Burundi wakati wa hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC)kwenye maonyesho ya utalii ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la
Mense Berlin jijini Berlin Ujerumani, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na
mkakati wa Kutangaza utalii wa Afrika Mashariki na mwaka huu ilikuwa na kazi
moja ya kunadi maajabu manne ya Afrika yaliyopatikana katika ukanda huu wa nchi
za Afrika Mashariki ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mto Nile, Mbuga ya wanyama ya
Serengeti na Ngorongoro Crater huku Tanzania ikiwa kinara kwa ukanda huu wa
Afrika Mashariki kwa maajabu yake matatu ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya
Serengeti na Ngorongoro Crater jambo lililofanya itamkwe mara nyingi miongoni
mwa viongozi waliopata nafasi kuzungumzia utalii wa Afrika Mashariki PICHA NA
FULLSHANGWEBLOG Kaimu Balozi wa Tanzania nchini
Ujerumani Christopher Mvula akipokea tuzo maalum iliyotolewa na iliyotolewa kwa
nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Bi Maria Mutagamba Waziri wa
Utalii wa Uganda katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki
kwenye maonyesho ya (ITB) Berlin jana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kulia anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC) Jesica
Eriyo Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Geofrey Meena kulia akiwa na Adolf Mchemwa Mkuu wa Utawala
Ubalozi wa Tanzania Ujerumani wakiwa katika hafla hiyo Bi. Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hotuba yake na kuzungumzia masuala
mbalimbali kuhusu utalii wa nchi za Afrika Mashariki Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) Bi Jesica Eriyo akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo ili
azungumze na washiriki wa maonyesho hayo pamoja na wageni waalikwa katika hafla
hiyo. Ken Nyauncho Osinde Balozi wa Kenya nchini
Ujerumani akizungmza na wageni waalikwa na kueleza ushirikiano wa Mabalozi wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani katika kutangaza utalii wa ukanda
huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kutoka Tanzania Bi Maimuna Tarishi akitambulishwa rasmi katika hafla
hiyo Maofisa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki
kutoka kulia ni Bw. MashauriBrenda Mugambi na Aileen Mallya wakiwa katika hafla
hiyo. Baadhi ya wageni kutoka taasisi
mbalimbali za kimataifa zinazojihusisha na masuala ya utalii wakiwa katika hafla
hiyo. Dk. Nyamajeje Wigoro kutoka EAC
akisalimiana na viongozi wawakilishi wa nchi za Jumaiya ya Afrika Mashariki
kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC) Bi. Jesica Eriyo.
Wageni mbalimbali ambao pia ni
washiriki wa maonyesho hayo ya utalii kutoka Uganda wakiwa katika hafla
hiyo. Kaimu Balozi wa Tanzania nchini
Ujerumani Chrisopher Mvula kushoto akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki katika hafla hiyo.
Dk Nyamajeje Wegoro akishauriana
jambo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda katikati ni
Bw. Mashauri kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki
Makatibu wakuu na Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki
wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi na maofisa wa Utalii wa Nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki
Makatibu wakuu na Mawaziri wa nchi za Afrika Mashariki
wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi na maofisa wa Utalii wa Nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki
Kikundi cha ngoma kutoka nchini
Uganda kikitumbuiza katika hafla hiyo. Kikundi cha ngoma kutoka Burundi
kikitumbuiza katika hafla hiyo
Wa kwanza ni Waziri wa Maliasili
Uganda B. Maria Mutagamba, Balozi wa Kenya nchini Ujerumani Ken Nyauncho Osinde
na Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Bi Maimuna Taarishi
wakishiriki kucheza ngoma ya Asili ya Uganda wakati wa hafla hiyo.
Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini
Ujerumani Christopher Mvula kulia akishiriki kucheza ngoma muziki na wageni
waalikwa mbalimbali katika hafla hiyo
Post a Comment