Jana
usiku, kampuni ya Magazeti ya Mwananchi Communications ilizindua
muonekano mpya wa gazeti lake la Mwananchi ambapo ilifanya halfa fupi
katika ukumbi wa Mlimani City, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbali
mbali wa kiserikali, vyama vya siasa, wafanyabiashara, wadau wa habari
na watu mbali mbali maarufu jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika
sherehe hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya Katiba, Balozi Joseph Sinde Warioba. Pichani juu anaonekana
Mheshimiwa Warioba(Wa pili kutoka kushoto, akishiriki katika zoezi la
uzinduzi wa gazeti hilo lenye muonekano mpya, pamoja na Mwenyekiti wa
bodi ya kampuni hiyo, Bi Zuhura Muro, huku Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo, Bw Tido Mhando(kushoto), na Meneja Biashara na maendeleo,
Bw Theophil Makunga(kulia) wakishuhudia
Mhariri Mtendaji wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, ambaye kwa sasa ni Meneja Maendeleo ya Biashara akieleza kwa kina kuhusiana na miaka 13 ya Gazeti la Mwananchi na mafanikio yake kwa waalikwa
Nasaha kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw Tido Mhando
MEZA
KUU: Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi,
Mgeni Rasmi Mh Warioba, na Mwenyekiti wa Bodi wa MCL Bi Zuhura Muro
wakiteta jambo
Mwenyekiti wa Bodi naye alisema machache
Mhariri
Mtendaji wa Gazeti la mwananchi, Bw Dennis Msacky(kulia), akiwa na
Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya MCL, Bakari Machumu na mtaalam wa
ubunifu wa kurasa Bi Kelly Frankeny
Uzinduzi rasmi...
..na huu ndio muonekano mpya!
Linapendeza kwa kweli
Umeona mwenyewe, hapa ni kila sehemu ya ndani imefanyiwa marekebisho
Picha na watu mashuhuri
Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma kaskazini pamoja na katibu mwenezi wa Chama Cha mapinduzi, Nape Nnauye wakiteta jambo
Meza kuu ilipata nafasi ya kuperuzi, ...na kudadisi...
Baadae kila mtu alipata nakala yake
Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi akitoa nasaha zake
kelly Frankey, mtaalamu wa miundo mbali mbali ya gazeti la mwananchi naye alipata wasaa wa kujieleza mbele ya wageni waalikwa
Kila mtu alifurahi
Mshereheshaji alikuwa Taji Liundi, moja kati ta wakongwe katika tasnia ya utangazaji
Baada ya yote, Skylight Band ikamaliza mambo kwa burudani ya Nguvu!Picha Zote Kwa Hisani ya Mdimu Blog
Post a Comment