Picha Juu na chini ni Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwapokea wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wanafunzi wa vyuo vikuu, Maprofesa, na wadau wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 uliofanyika jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 – Kuchomoza kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti iliyopita.
Hata hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima ujumla wa maendeleo katika Jamii.
Bw. Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela.
Lakini pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha.
Aidha amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu nyingine duniani.
Baadhi ya Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakimsikiliza Dkt. Alberic Kacou (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 iliyofanyika jijini Dar leo.
Mshauri wa Uchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara akiwasilisha ripoti hiyo na kuifafanua ambapo ameeleza kuwa Nchi za Kusini zinakabiliwa na changamoto ambazo pia inazikabili nchi zilizoendelea za Kaskazini, ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wazee, shinikizo kwenye mazingira, tofauti za kimaisha katika jamii, kukosekana kwa uwiano kati ya maandalizi ya kielimu na nafasi za kazi na umuhimu wa ushirikishwaji umma na mengineyo, akisena hayo yanahitaji ufumbuzi wa kitaifa na kimataifa ikiwa nchi zinazoendelea zinataka kuendeleza kasi yao ya maendeleo.
Bw. Amarakoon amesema Ripoti hiyo inaonya kuwa namba ya watu walio maskini sana inaweza kuongezeka kufikia watu bilioni tatu ifikapo mwaka 2050, labda tu kama hatua za pamoja kimataifa zitachukuliwa kuzuia maafa ya kimazingira.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akikata utepe kuzindua rasmi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akiwa na Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sasa imezinduliwa rasmi.

Mmoja wa mabalozi akiperuzi Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 baada ya kuzinduliwa rasmi.
Ripoti ya mwaka 2013 inasema kuchomoza kwa Nchi za Kusini ni changamoto kwa taasisi duniani kubadilika na kunaonyesha njia mpya ambazo nchi na maeneo yanaweza kufanya kazi pamoja kukabiliana na changamoto zinazofanana.
Wakati taasisi kongwe haziendi na mabadiliko, taratibu mpya zinatokea, ikiwamo mitandao mipya ya ushirikiano ya kitaifa na kimataifa zikiwemo jumuiya za kibiashara, jumuiya za kiulinzi, benki za maendeleo na makubaliano ya nchi kwa nchi.
Baadhi ya Waheshimiwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini wakishuhudia uzinduzi wa Ripoti hiyo.
Mwakilishi wa UN Women Tanzania Bi. Anna Collins-Falk.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mollel Raphael Leckshon akitoa maoni yake juu ya Ripoti ya Maendelo ya Dunia 2013 iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Prof. Delphin Rwegasira kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akichangia maoni yake baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa.
Wageni waalikwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini katika uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013.
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Bw. Phillipe Poinsot akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na baadhi ya waheshimiwa mabalozi baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Dunia 2013.
Sangita Khadka wa Ofisi ya RCO (kushoto) na Stella Vuzo wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Dunia 2013 iliyozinduliwa rasmi jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.
Kansela wa Ubalozi wa Yemeni nchini Bw. Mohammed Abdulah Al-Dhaifi(kulia) akibadilishana business card na Mshauri wa Uchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara mara baada ya uzinduzi huo.