TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete leo Ijumaa 15 Machi, 2013 mchana amemtumia salamu za Pongezi Baba
Mtakatifu Francis I kwa kuchaguliwa kwake kuwa Papa wa kanisa Katoliki Duniani
na Vatican.
“Kuchaguliwa kwako ni ushuhuda tosha wa imani na
heshima kubwa ambayo kanisa Katoliki inayo kwako, historia yako na upendo wako
wa kujali na kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa
wakatoliki, wasio wakatoliki na wasio wakristo pia kusherehekea uteuzi
wako” Rais Kikwete amesema kwenye barua
yake ya Pongezi kwa Papa Francis I.
Vatican na Tanzania
imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete amemhakikishia Papa
Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia utaimarika zaidi chini ya
uongozi mpya wa Papa Francis I
“Mwisho”
Imetolewa
na:
Premi
Kibanga
Mwandishi wa Habari wa
Rais, Msaidizi,
IKULU
DAR ES
SALAAM
15 March,
2013
Post a Comment