Meneja wa QX,Ally Abdalah (kulia) na Mpishi Mkuu wa
Bar hiyo, Emanuel Seneyo (wa pili kushoto) wakionyesha kitita cha shilingi
milioni moja baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe
Munasa(wa pili kushoto) ikiwa ni mabingwa wa Safari Nyama
Choma Mkoa wa Arusha yalifanyika katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa
wiki.Wa pili kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo,Meneja
Mauzo wa Kanda, Kitio Wilderson na mhudumu wa Bar ya QX akishangilia kwa
furaha.
Meneja wa QX,Ally Abdalah(kulia) na Mpishi Mkuu wa Bar
hiyo, Emanuel Seneyo(wa pili kushoto) wakionyesha kitita cha shilingi milioni
moja baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munasa(kushoto)
ikiwa ni mabingwa wa Safari Nyama Choma Mkoa wa Arusha yalifanyika katika
viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.Wa pili kulia ni Meneja wa Bia ya
Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja Mauzo
wa Kanda, Kitio Wilderson.
Mashabiki wa Bar ya QX ya
Arusha wakishangilia na Meneja, Ally Abdalah (wa pili kulia) mara baada ya
kutangazwa mabingwa wa Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha yaliyofanyika
katika viwanja vya General Tyre mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu,
Arusha
QX Pub, wametwaa ubingwa wa
mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Aresha, baada ya kuzigaragaza baa nne
zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo
katika fainali zilizofanyika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa General Tyre, baa
hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja pamoja na
cheti.
Post a Comment