Na.Mo Blog Team.
 
Serikali nchini imetakiwa kuacha kufanya mambo bila kutaka ushauri katika masuala ya kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitalii na badala yake ikae meza moja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata muafaka wa kweli na ikibidi ivipe ruzuku ili kuhakikisha uendeshaji wa vituo hivyo katika mfumo huo mpya unafanikiwa.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (pichani), ameitaka Serikali ikubali kwa nia njema kabisa angalau kwa muda wa miezi sita ijayo au hata mwaka mzima ujao kwa mikoa mitatu, kutumia mfumo wa analojia kwa kuwa ndio walikuwa wamejiandaa nao na ndio walikuwa wamesajili nao vyombo hivi ili kujiandaa kuingia kwenye digitali.
Hata hivyo serikali yenyewe imeshatoa tamko kwamba haitorudia nyuma kwenye mfumo wa analojia na badala yake itaendelea kusonga mbele katika mfumo wa digitali kwani tayari mfumo huo ni mfumo wa kiulimwengu.
Suala hilo limeleta changamoto kubwa na wadau mbalimbali wa masuala haya ya habari ambao wametaka kuwepo na mazungumzo ili kuweza kufikia muafaka mzuri katika uendeshaji wa vyombo hivi vya habari kwa kuwa wenyewe wanaona ni mzigo mkubwa kwa sasa kuingia katika mfumo huo wa digitali.