Ubao wa Matokeo unavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Timu ya Taifa ya Morocco uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka Golikipa na Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil, uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda Bao 3 – 1, mabao yaliyotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari, Mbwana Samatha. Kwa hisani ya Michuzi Blog