Waziri
mkuu Mizengo Pinda (mwenye miwani) akisaidiwa kutundika mzinga wa
kisasa na naibu waziri wa mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu
(kushoto) na mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone, kwenye
maadhimisho ya utundikaji mizinga kitaifa uliofanyika katika kijiji cha
Aghondo Manyoni Magharibi.
Waziri
mkuu Mizengo Pinda, akihutubia kwenye kilele cha utundikaji mizinga
kitaifa uliofanyika katika kijiji cha Aghondi jimbo la Manyoni
magharibi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.Mary Nagu,
akitoa nasaha zake kwenye kilele cha utundikaji mizinga kitaifa
uliofanyika katika kijiji cha Aghondi jimbo la Manyoni magharibi.(Picha
zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amewaagiza
watendaji na viongozi mbalimbali, kuhamasisha vijana kujiunga/kuanzisha
vikundi vya ufugaji nyuki ili waweze kupambana vema na umaskini pamoja
na uhaba wa ajira.
Mh.
Pinda ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kilele cha siku ya
utundikaji mizinga kitaifa uliofanyika katika kijiji cha Aghondi jimbo
la Manyoni Magharibi.
Amesema kazi ya ufugaji wa nyuki ni rahisi mno na ni tofauti na shughuli zingine za kiuchumi ikiwemo ya kilimo na ufugaji.
Waziri
Mkuu amesema pamoja na urahisi huo, lakini ndiyo kazi nzuri ambayo ina
uwezo mkubwa wa kumkomboa mhusika kiuchumi, kwa madai kwamba mazao ya
ufugaji nyuki, yana soko zuri la uhakika wakati wote.
Mh.
Pinda amesema kwa hali hiyo, upo umuhimu mkubwa kwa watendaji na
viongozi kuhamasisha vijana kwa bidii, ili waweze kujiunga katika
vikundi na kwa njia hiyo watakuwa wamejijengea mazingira mazuri ya
kuweza kupewa misaada mbalimbali ikiwemo ya kuwawezesha kufuga nyuki.
Katika hatua nyingine Waziri mkuu almesema ufugaji wa nyuki utasaidia sana kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
Amesema
kutokana na ukweli huo mazingira yakitunzwa vizuri na kulindwa pamoja
na mambo mengine, nchi itarudi kwenye neema ya mvua zenye kheri.
Post a Comment