Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakifanya mahojiano na mtangazaji wa Radio Vatican, Padri Richard Mjigwa (katikati) kweye moja kati ya studio za Raido hiyo Mjini Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Picha juu na chini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakiongozwa na Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa Benedikti, Roma kutoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma walikohudhuria sherehe za kumsimikwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 kwenye viwanja vya Kanisa hiloMachi 19,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakipata maelezo kuhusu historia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma kutoka kwa Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa wa Benedikti, Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Machi 202013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula (FAO), Jose Graziano da Silva wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Roma, Machi 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula , FAO, Bw. Jose Graziano da Silva kutia saini katika kitabu cha wageni mshuhuri wakati alipotembelea Ofisi za FAO mjini Rome Machi 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva baada ya mazungumzo yao wakati alipotembelea makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).