Naibu waziri wa nyumba,ardhi na
makazi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi,Goodlucky Ole
Medeye amezitaka Serikali za Mitaa ukiwemo Uongozi wa Vijiji Mbalimbali
ndani ya jimbo hilo kuhakikisha kuwa kamwe hawaangilii shuguli au miradi
mbalimbali ya Wafadhili ambayo ina malengo ya kuwasaidia wananchi
Medeye aliyasema hayo Jimboni
humo wakati akizundua zahanati ya Ester iliopo katika Kijiji cha
Ngaramtoni ambayo ilijengwa kwa nguvu za wafadhili kutoka nchini
Uingereza kwa malengo ya kudumisha sekta ya afya hasa afya ya mama na
mtoto
Medeye alisema kuwa kuwa endapo
kama Vijiji vitakuwa vinaingilia masuala ya Miradi ambayo imetolewa na
wafadhili kwa malengo mbalimbali ni wazi kuwa malengo hayo yatakwama na
badala yake umaskini ndio utakaokirhiri huku jamii ikibaki na mateso
mengi
Aliongeza kuwa kazi ya Serikali
ya Kijiji ni kuhakikisha kuwa miradi hiyo inafanya kazi kwenye viwango
vya hali ya juu kama yalivyokuwa malengo ya wafadhili hivyo kama
Serikali za kijiji zitafanya hivyo basi zitachangia sana mabadiliko tena
ya hali ya juu huku mabadiliko hayo yakichangia kupungua kwa umaskini
Akiongelea Mradi huo wa zahanati
ambao utaweza kuwanufaisha wananchi zaidi ya elfu kumi alisema kuwa
mbali na kuwanufaisha wananchi wa Kijiji hicho cha Ngaramtoni lakini pia
utaweza kuwanufaisha wananchi wa jimbo hilo kwa ujumla hivyo baadhi ya
wanasisasa wasitumie nafasi hiyo kwa kuwadanganya watu kuwa kuna ubaguzi
baina ya watu na watu
Awali wanawake ambao ndio
walengwa wakubwa sana wa mradi huo walisema kuwa zahanati hiyo itaweza
kuwasaidia kwa kuokoa afya zao kwani walikuwa wanalazimika kutembea
Umbali wa zaidi ya Kilomita Kumi kwa ajili ya kutafuta huduma za afya
hali ambayo wakati mwingine husababisha vifo
Post a Comment