
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na
Mwakilishi wa JICA nchini Yasunori Onishi (kulia) wakibadilishana hati za
mkataba wa Japan kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji
safi na salama katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.

Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) na Balozi
wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Japan
kusaidia shilingi bilioni 1.28 kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama
katika baadhi ya vijijini vya mkoa wa Tabora.
---
Serikali ya Japan kupitia Shirika la JICA imesaini
mkataba wa kuisaidia Tanzania shilingi Bilioni 1.28 za kusaidia usambazaji
maji katika mkoa wa Tabora .
Fedha hizo zimetolewa leo(jana) na Balozi wa Japan
nchini Tanzania Mh. MASAKI OKADA katika sherehe iliyofanyika jijini Dar es
salaam.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Tanzania Waziri wa
Fedha Mh. Dkt. William Mgimwa alisema msaada huo utasaidia kupunguza kero ya
upatikanaji wa maji katika baadhi ya vijiji mkoani Tabora na pia kukabiliana na
vita dhidi ya umaskini.
‘’Ninafurahi ya kuona kwamba makubaliano ya msaada huu
tulio saini hivi punde utaiwezesha serikali yako ya Japan kupitia kampuni ya
JICA kutupatia fedha za Kijapan Yeni 76 milioni sawa na shilingi bilioni 1.28 za
kitanzania, kwaajili ya kusaidia utekelezaji wa usamabazaji maji vijijini katika
mkoa wa Tabora”. Mh. Dkt, Mgimwa alisema.
Aidha Dkt Mgimwa kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya
Tanzania aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada wake huo muhimu ambao umekuja
muda muafaka wakati Tanzania iko katika mapambano dhidi ya umaskini ikiwemo
kuhakikisha wanapata maji safi na salama.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania Mh,
MASAKI OKADA alisema kuwa Japan tangu mwaka 1996,inatekeleza miradi sita ya
maji katika mikoa ya Kagera ,Singida, Manyara , Shinyanga ,Mwanza , Mara, Mtwara
, Lindi, Pwani , Dar es Salaam pamoja na Zanzibar.Alisema kuwa hadi hivi sasa
jumla ya watu laki nane na sitini elfu wamenufaika na miradi hiyo hapa nchini
Tanzania.
Japan na Tanzania
zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu ambapo hadi hivi sasa uhusiano wa Nchi
hizo umedumu kwa muda wa miaka 50
Na
Benedict Liwenga
Idaya ya Habari Maelezo-Dar es
Salaam
Post a Comment