Ndugu Abdurahman Kinana Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM akitembelea shamba darasa la wananchi wapatao 180 kutoka Wilaya ya Morogoro Vijijini wanaosimamiwa na kupewa mafunzo ya kilimo bora na ufugaji bora na Shirika la Maendeleo la Korea KOICA, wakati alipotembelea mradi huo katika ziara yake ya kichama ya mkoa wa Maorogoro, ambapo leo alifanya ziara katika Wilaya ya Morogoro vijijini na kufungua mashina na matawi ya chama hicho huku akipokea wanachama wapya waliojiunga na waliotoka vyama vya upinzani, Kulia anayezungumza na Abdurahman Kinana ni Kim Sun Ho Meneja Mradi huo wa KOICA Korea, Wananchi hao wanamiliki zaidi ya hekari 150 kila mmoja ana magunia 8 ya mahindi waliyovuna mwaka jana huku wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 50,ooo,ooo benki.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG) 

Mratibu wa mradi huo Mbwambo Apendaimani akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana juu ya utaalamu unaotolewa na shirika hilo kwa wakulima hao na ufugaji wa kisasa, Katikati ni Kim Sun Ho Meneja Mradi
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akitembelea majengo yatakayotumika katika mafunzo ya ufugaji darasa kwa wananchi katika mradi huo. 

Hapa akipata maelezo huku akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa CCM taifa na mkoa wa Morogoro. 

Katibu mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akifungua shina la wakereketwa la Tekemelo Kiroka Morogoro vijijini
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM Kata
ya Kiroka.
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akipokea kadi na bendera kutoka kwa aliyekuwa Katibu Kata wa Chadema Kisemu Bwana Raurent Costantine aliyejiunga na CCM 

Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akifurahia zawadi ya majogoo mawili aliyopewa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Lucy Nkya 

Hapa akifungua tawi la Msala
Akitembelea mahali patakapojengwa soko katika Kata ya Makuyuni Matombo Morogoro 
Akitembelea mahali patakapojengwa soko katika Kata ya Makuyuni Matombo Morogoro 
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akichanaganya mchanga na simenti wakati alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Makuyuni Morogoro vijijini Leo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Dk Sayuni Robert mganga mkuu wa kituo cha afya cha Mauyuni 

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Lucy Nkya juu ya ujenzi wa majengo ya kituo cha Makuyuni.
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akikabidhiwa zana za kimila na Chifu Kingaru wa Uruguru huku akiwa amekaa kwenye kigoda 

Wanachama wapya wa CCM wakionyesha kadi zao juu baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana. 

Kila jambo halikosi vituko huyu mzee alionekana yuko makini sana akichukua picha wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akifanya moja ya shughuli za kufungua shina katika ziara yake Wilayani Morogoro Vijijini huko Mvuha Matombo 

Katibu wa NEC Oganizesheni CCM Dk. Mohamedapo Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa Mvuha Matombo hawapo pichani , kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa morogoro Kusini Innecent Kalogeres. 

Wananchi wa Kata ya Mvuha Matombo wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye wakati akiwahutubia. 

Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akikabidhi kadi kwa mwanachama mpya wa chama hicho Eliza Rashid katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mvuha Matombo. 

Wanachama wapya wa CCM wakionyesha kadi zao mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdurahman Kinana.





Post a Comment