baadhi ya wanafunzi
wakifanya mafunzo ya ukocha kwa vitendo yaliokuwa yakiendeshwa na kituo cha
International Insparation kanda ya kaskazini kwenye viwanja vya sheikh Amri
Abeid jijini Arusha.
picha ya pamoja baada ya
kumaliza mafunzo yao wakiwa na nyuso za furaha baada ya kutunukiwa vyeti na
katibu wa baraza la michezo la taifa Henry Lihaya kwenye uwanja wa Seikh Amri
kalita Abeid.
******
Na Mahmoud Ahmad
Arusha
Mafunzo ya michezo
shirikishi kwa jamii ya kukuza vipaji na michezo yaliokuwa yakindeshwa na kituo
cha kuendeleza vipaji na michezo cha International Insparation kanda ya
kaskazini kwa wiki moja na kuwashirikisha zaidi ya walimu na wanafunzi 70
yamefungwa jana jijini hapa na katibu wa BMT.
Akifunga mafunzo hayo
katibu mkuu wa baraza la michezo la taifa Henry Lihaya aliwataka wanafunzi hao
kujituma na kujijenga kwenye masuala ya kimichezo kwani kwa sasa michezo ni
ajira tosha.
Huku akiwataka kuyatumia
vizuri mafunzo hayo kwa manufaa ya taifa na kujenga miili yao sanjari na kupiga
vita maambukizi ya magonjwa ya ukimwi na Malaria kupitia michezo watakayoenda
kufundisha.
“Ndugu zangu vijana
mkumbuke hivi sasa michezo ni ajira na mafunzo mtakayopata yatawajengea uwezo na
msikae nayo muende mkafundishe kama mlivyofundishwa ilikupiga vita matumizi ya
madawa ya kulevya na maradhi muwe mabalozi wazuri huko muendako”alisema
Lihaya
Nae Mratibu wa
Internation Inspiration mkoa wa arusha ambao wameratibu Mafunzo hayo Samwel
Mpenzu alisema kuwa mafunzo hayo yaliwashirikisha zaidi ya walimu30 na wanafunzi
30 kutoka halmashauri ya jiji la Arusha na yalihusu kozi ya ukocha wa michezo
mbali mbali ikiwa ni muendelezo wa kusogeza michezo kwa vijana.
Mpenzu alisema kuwa
Ujumbe wa mafunzo hao ulikuwa ni michezo kwa Afya na kuwa mbali na mafunzo ya
ukocha pia waliwafunza kujikinga na maambukizi ya maradhi wakiwa michezoni
sanjari na ushirikishi wa jamii katika kukuza michezo hapa
nchini.
“Unajua kuwa michezo ni
huduma muhimu hivyo yatupasa kuwasogezea jamii kupenda michezo katika kupiga
vita maradhi mbali mbali yanayoiandama jamii”alisema Mpenzu.
Aidha mwalimu wa mchezo
wa riadha Francis John alisema kuwa katika mchezo huo alikuwa na wanafunzi zaidi
ya 21 na walijifunza jinsi ya kutupa mitupo,Miruko,na Mbio na wote walifanikiwa
kumaliza mafunzo hayo.
Mwanafunzi wa shule ya
sekondari Felex Mrema Greygory John 15 alisema kuwa pamoja na kupata mafunzo
hayo atayatumia vizuri kataka kuendeleza michezo hapa jiji na mkoani huku
akiwataka vijana wenzake kuacha kutumia madawa ya kulevya kwani ni hatari kwa
afya zao na huharibu maisha.


Post a Comment