Mwili wa marehemu, Romanus
Masige mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro ukiwa umelala chini katika barabara
ya Old Dar es Salaam eneo la maktaba ya mkoa wa Morogoro baada ya kudaiwa
kusukumwa na wenzake waliokuwa nao wamepakiwa nyuma ya lori wakati wakisafiri
kutoka Kihonda kuelekea kituo kikuu cha polisi mjini hapa.(Picha na Jackson Audiface)
Shuhuda akieleza
tukio zima lililotokea
Mwili wa marhemu Masige ukiwa
umefunikwa kwenye eneo la tukio
Hili gali ndilo
lililomkanyaga marehemu
Msamalia akimwaga mchanga kwenye damu ya mtu aliyekanygwa na gari
.......................
Msamalia akimwaga mchanga kwenye damu ya mtu aliyekanygwa na gari
.......................
Mashuhuda ambao walishuhudia tukio hilo walitudokeza kuwa nyuma ya lori hilo ilikuwa imebeba
kokoo na abiria wawili na mara baada ya kufika eneo hilo alionekana moja wao
akimsukuma marehemu aliyedondoka chini na gurudumu la nyuma lilimkanyaga na
kupoteza maisha papo hapo huku mwenzake baada ya gari kusimama alichukua
baiskeli na kutoweka eneo wakati dereva akijisalimisha kituo cha
polisi.
"Alikanyagwa kichwani huyu marehemu na hilo lori baada ya
kusukumwa na mwenzake na gari iliposimama alichukua baiskeli na kutoweka eneo
hilo hatukuwezakuelewa nini kinaendelea". Kilisema Chanzo
chetu.
Habari hizi kupitia blog hii iliendelea kudokezwa kuwa
mkasa huo kwa marehemu huyo ulitokana na kitendo chake cha kupiga bosi wake
kuuziwa kokoto hizo mara mbili jambo ambalo hakukubaliana nalo na kuwaona
wahusika waliopeleka kokoto hizo kuwashuku kuwa ni wezi ndipo safari ya
kuwapeleka kituo kikuu cha polisi na kabla hajafikiwa kituo tukio hilo likatokea
majira ya saa 10 jioni jana.
Marehemu Masige ni mkazi wa Kihonda akiwa ni mwenyeji wa mkoa wa
Kigoma ambapo taarifa zilizotufikia punde zinasema kuwa mwili wa marehemu huyo
utasafirishwa kwa ajili ya mazishi mkoani
Kigoma.
Masigealikuwa Mwali wa kwaya katikan kanisa katoliki
kigango cha kristo mfalem na mlinzi katika kanisa
hilo.
Mungu ailaze mahala pema peponi Amina
Post a Comment