Arusha: Kushikiliwa kwa
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema (pichani) kumeendelea kuibua sokomoko
baina ya polisi kwa upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa
upande mwingine.
Arusha. Lema aliyekamatwa
usiku wa manane kuamkia Ijumaa wiki hii, alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika
Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha lakini alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba
kuachiwa kwake kungehatarisha amani.
Akizungumza na gazeti hili
kabla ya kujisalimisha kwa askari hao usiku huo wa kuamkia juzi, Lema
alithibitisha kuwapo kwa polisi nje ya nyumba yake:
“Wapo nje ya nyumba yangu,
wanatishia kupiga mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi
wangu na mimi nimewataka wanipe hati ya
kunikamata,”alisema.
Wakili wa Lema, Humphrey Mtui
alisema mahojiano ya mteja wake na polisi yalidumu kwa zaidi ya saa tatu kuanzia
saa 7:50 mchana hadi saa 11:15 jioni, na kwamba walitaka ufafanuzi kwenye hoja
tatu walizodai kwamba zilijengwa kwenye kauli alizotoa Lema wakati alipokuwa
akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Arusha
(IAA).
Maneno hayo yanayotafsiriwa
na polisi kuwa ni uchochezi ni pamoja na “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote
duniani ni woga” na “Nimepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 Mkuu wa Mkoa
atafika, asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya
msingi ya kupatiwa ulinzi.”
Kauli nyingine ni “Hawa ndio
viongozi wetu (akimaanisha mkuu wa mkoa), tunaowategemea wanakuja kwenye
matatizo wakijivuta utafikiri wanakwenda kwenye
send-off.”
Lema anadaiwa kutamka maneno
hayo baada ya Mulongo kugoma kuzungumza na wanafunzi kisha kurejea ndani ya gari
akitaka viwepo vipaza sauti, kitendo kilichowafanya wanafunzi kuanza kumzomea
kabla polisi kuanza kulipua mabomu ya machozi na kumwondoa eneo la tukio mkuu
huyo wa mkoa.
Lema na Mulongo wote
walikwenda IAA kutokana na tukio la kuuawa kwa kuchomwa kisu kwa aliyekuwa
mwanafunzi wa taasisi hiyo, Henry Kago.
Baada ya vurugu hizo Mulungo
alimtuhumu Lema kuandaa mazingira ya yeye kuzomewa .
Wakati hayo yakiendelea,
askari katika kituo anakoshikiliwa Lema jana asubuhi walivutana vikali na ndugu
wa mbunge huyo pamoja na uongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha baada ya kumpa dakika
moja kunywa chai aliyoletewa na kukataa asipewe dawa ya meno kutoka kwa mkewe,
Neema.
Habari ambazo gazeti hili
lilizipata zinasema kutokana na hali hiyo, uongozi wa Chadema ulilazimika
kumtuma wakili wa Lema, Method Kimomogoro kwenda Kituo cha Kati cha Polisi
Arusha kujua sababu za polisi kufanya hivyo.
MWANANCHI
Mmoja wa ndugu wa Lema
alisema polisi walimpa mbunge huyo dakika moja tu kunywa chai na kwamba muda huo
ulipokwisha walimwongezea dakika nyingine tatu na kwamba zilipomalizika
walimwamuru arejee mahabusu.
Wakati polisi wakifanya
hivyo, tayari walikuwa wamekataa asipewe dawa ya meno aliyopelekewa na mkewe,
Neema na kwamba matukio hayo yalizua mvutano mkali baina yake (Lema) na polisi
waliokuwa kituoni hapo.
Mdee, Nassari kukutana na
Mulongo
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Nassari aliliambia gazeti
hili jana kwamba wameamua kutoka Dodoma hadi Arusha kwa ajili ya “kushughulikia
suala hilo.”
“Jumatatu tunatarajia kuonana
na mkuu wa mkoa na tayari nimempa taarifa. Tunataka kuzungumza naye kilichotokea
na hali ya kisiasa kwa sasa Arusha,”alisema Nassari.
Alisema wao kama wabunge,
hawawezi kukaa kimya wakati kunaonekana kuna mgogoro baina ya mkuu huyo wa mkoa
na mbunge mwenzao, Godbless Lema ambao unakiuka haki za
kibinadamu.
“Tutazungumza naye na tutatoa
ushauri wetu …na mimi kama mbunge wa Mkoa wa Arusha, nadhani nina nafasi ya
kushauriana na mkuu wa mkoa kuhusiana na hali ya mambo ilivyo sasa
Arusha,”alisema Nassari na kuongeza:
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
Hata hivyo, juhudi za kumpata
jana mkuu wa Mkoa wa Arusha, kuelezea kama amepokea ujumbe kutoka kwa wabunge
hao, zilishindikana kutokana na kuwa katika mapokezi ya marais watano wa nchi za
Afrika ya Mashariki.
Chadema kumzomea RC
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katibu wa Chadema, Kanda ya
Kaskazini, Amani Golugwa alisema wafuasi wa chama hicho wataendelea kumzomea
Mulongo kila watakapomwona hadi pale atakapobadilika kifikra, kimwenendo, maneno
na vitendo kuhusiana na uhalali wa Chadema na viongozi wake katika uongozi wa
umma waliokabidhiwa kisheria.
“Kama kupigiwa makofi na
kushangiliwa anapofanya vyema kazi yake,
vivyohivyo mkuu wa mkoa
ategemee kukumbana na zomeazomea kubwa kuliko aliyopata Uhasibu iwapo
hatabadilika kiutendaji kwa kufanya kazi za kisiasa badala ya kuhudumia umma
wote bila kujali tofauti za kiitikadi kisiasa,” alisema
Golugwa.
Katika mkakati wake, Chadema
kimetishia kumburuta mahakamani Mulongo kwa tuhuma za kuzusha uongo na kumtishia
Lema kwa maneno makali.
“Mawakili wetu wanaendelea na
utaratibu wa kufungua kesi ya kumshtaki mkuu wa mkoa kwa kosa la kumtishia kwa
maneno makali Lema na pia kutoa maneno ya uzushi, upotoshaji na uongo,”alisema
Golugwa.
Chadema pia walisema askari
polisi waliomkamata Lema hawakuwa na kibali cha ofisi ya Spika wala hati ya
kukamata kutoka kwa ofisa wa jeshi hilo kama sheria
inavyoelekeza.
CCM Arusha
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.
MWANANCHI
Post a Comment