
Mfanyabiashara wa Mbeya ambae ndie alikuwa dereva wa gari namba T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na kusababisha kifo cha askari mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko wakati wa msafara wa Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam hivi karibuni , akifikishwa mahakama ya Mwanzo Bomani Iringa jana kwa tuhuma za kujipatia gari aina ya fuso yenye tmanani ya Tsh milioni 30 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mwanamke Venannsia Sanga wa Iringa (Picha na Francis Godwin)
Na Francis Godwin, Iringa
MFANYABIASHARA mkazi wa Mbeya ambae alikuwa
akiendesha gari lenye namba za usajili T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na
kusababisha kifo cha askari mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko wakati wa
msafara wa Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam ,amefikishwa mbele ya
hakimu wa mahakama ya Mwanzo Bomani mjini Iringa kwa tuhuma za kujipatia gari
lenye thamani ya Tsh milioni 30 .
Akisoma shtaka hilo hakimu wa mahakamani
hiyo ya Mwanzo Bomani Mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo
anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 4 mwaka 2012 katika eneo la Miyomboni
mjini Iringa .
Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya
kutenda kosa hilo alitoweka na kujificha katika mikoa mbali mbali hapa nchini
.
Hata hivyo alisema kuwa mlalamikaji katika
shtaka hilo baada ya jitihada za kumtafuta kushindikana ndipo alipofika
mahakamani Februari 15 mwaka huu kufungua kesi namba 61 /2013 kuhusiana na
mtuhumiwa huyo.
Alisema kuwa kutokana na kufunguiliwa kwa
kesi hiyo jeshi la polisi kwa kushirikiana na mlalamikaji waliendelea kumsaka
mtuhumiwa huyo bila mafanikio na baada ya kutokea ajali iliyosababisha kifo
cha askari huyo wa usalama barabarani jijini Dar es Salaam katika msafara wa
Rais Kikwete ndipo mtuhumiwa huyo alipokamatwa baada ya picha yake kuonekana
katika vyombo vya habari .
Mtuhumiwa huyo amekana kosa hilo ambapo
mahakama hiyo imesema kuwa dhamana yake ipo wazi na kuwa mdhamini anapaswa
kusaini hati ya dhamana ya yenye thamani ya Tsh. milioni 15 masharti ambayo
yalitimizwa na wadhamini na mfanyabiashara huyo kutolewa kwa dhamana hadi
Aprili 25 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Wakati huo huo ndugu wa mfanyabiashara huyo
walionyesha kuwazuia wanahabari kumpiga picha wala kuandika habari hiyo
kwa madai kuwa ni habari ndogo ambayo jamii haipaswi kuijua na kumtaka
mfanyabiashara huyo kujifungika sura yake na kuondoka na msafara wa magari
mawili ya kifahari katika mahakamani hiyo .
Post a Comment