 |
Ndugu, Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati ulipowasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarishoya mazishi yatakayofanyika kesho Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. |
 |
Gari
lililokuwa limeubeba mwili wa msanii mkongwe wa muziki wa tarab, marehemu Fatuma
Binti Baraka 'Bi. Kidude', likiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani na
kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi yatayofanyika kesho
mchana katika Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha
zote kwa hisani ya Othman Maulid wa
ZanZinews) |
 |
Mwili
wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa
taratibu za mazishi yatakayofanyika kesho mchana na Kijiji cha Kitumba, Wilaya
ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. |
 |
Ndugu,
Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati ulipowasili
nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarishoya mazishi yatakayofanyika kesho Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya
Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. |
 |
Mrajisi
wa Baraza la Sanaa la Zanzibar, Khadija Batashi, akizungumza na waandishi wa
habari jinsi alivyoupokea msiba wa msanii mkongwe wa muziki wa taraba nchini, Bi
Kidude. |
 |
Matayarishi
ya mazishi ya msanii wa muziki wa tarab, Bi. Kidude yakiendelea nyumbani kwake
Rahaleo, mjini Zanzibar. |
 |
Mjukuu
wa Bi. Kidude Omar Ameir, akiwasiliana na jamaa kwa ajili ya kuwajulisha msiba
wa marehemu Bi. Kidude, baada ya mwili wa marehemu huyo, kuwasili nyumba kwake
kwa ajilimatayarisho ya mazishi yatakayofanyika kesho mchana baada ya Swala ya
Adhuhuri, ambapo atazikwa Kitumba. |
 |
Bi.
Maryam Hamdani akilakiwa na Bi. Sihaba wakati akiwasili nyumbani kwa marehemu
Bi. Kidude Rahaleo, mjini Zanzibar akiwa na
majonzi. |
 |
Waandishi
wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi. Kidude, Maryam Hamdan,
kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na mratibu wa safari
za Bi. Kidude nje ya nchi na katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akihudhuria
nje ya nchi wakati wa uhai wake. |
 |
Meneja
wa Sauti ya BUSARA Zanzibar, Stella Steven, akizungumza na waandishi wa habari,
mjini Zanzibar kwenye msiba huo, kuhusiana na marehemu Bi. Kidude ambaye alikuwa
akidhaminiwa na Sauti za BUSARA katika matamasha mbalimbali yaliokuwa
yakiandaliwa na taasisi hiyo ya sanaa, jinsi walivyopokea kifo chake kwa
masikitiko makubwa na kuacha pengo katika tasnia ya muziki wa taarab asilia
Zanzibar.
From:Jestina-George |
on Wednesday, April 17, 2013
Post a Comment