|
BAADHI
YA WANANCHI WAKIUANGALIA MWILI WA MTOTO LISTA PORINI KABLA POLISI HAWAJAFIKA
ENEO LA TUKIO |
|
SAMAHANI
KWA PICHA HII HATUJAIONYESHA VIZURI SABABU MWILI WA MTOTO LISTA UMEHARIBIKA
VIBAYA HIVYO TUMEONA SI VYEMA KUUONYESHA
WOTE |
|
MARA
TU BAADA YA POLISI KUUTOA MWILI PORINI NA KUUCHUNGUZA WALIWAKABIDHI WAZAZI ILI
WAENDELEE NA TARATIBU ZA MAZISHI YA MTOTO
LISTA |
|
MGUU
WA MAREHEMU LISTA |
|
MWANA
USALAMA AKIWA AMEUSHIKA MGUU WA MTOTO LISTA MARA TU BAADA YA KUUPATA MWILI WAKE
PORINI NA KUKUTA HANA BAADHI YA VIUNGO VYAKE VYA
MWILI |
|
UMATI
MKUBWA ULIOHUDHURIA MAZISHI YA MTOTO LISTA |
|
IMANI za kishirikina
zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange na Kata ya Isange baada ya matukio ya
kupotea na kuawa kwa Watoto kutokea mara kwa mara ambapo Marehemu hukutwa wakiwa
na mapungufu ya viungo ikiwemo Kichwa.
Katika tukio la hivi
karibuni Mtoto mmoja aliyejulikana kwa Jina la Lista Sebule (8) Mwanafunzi wa
Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mpombo iliyo katika Kata ya Isange
Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe Mkoani hapa ambaye alipotea katika
mazingira ya kutatanisha na kukutwa baada ya Siku 9 akiwa
amekufa.
Kwa mujibu wa mashuhuda
wa tukio hilo akiwemo Mama mzazi wa Marehemu Christina Sakalile alisema binti
yake alipotea majira ya saa tisa jioni Machi 31, Mwaka huu baada ya kutumwa
kupeleka simu kibandani ili kuchaji lakini hakurudi hadi Saa Kumi na Mbili jioni
hali iliyozua wasiwasi na kuanza kumtafuta bila
mafanikio.
Alisema baada ya tukio
hilo walitoa taarifa Kijijini ambapo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange Daudi
Nsyani ambaye baada ya kupewa taarifa hizo pia aliwataarifu viongozi wa Kata
akiwemo Diwani wa Kata ya Isange Elias Mwasandele na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo
Brayson Nguro ambaye aliitisha Mkutano wa
wananchi.
Mtendaji huyo
aliwaambia wananchi hao kushirikiana ili Mtoto apatikane hali ambayoiliitikiwa
na wananchi ambayo walitaka Mtoto apatikane aidha akiwa mzima ama Mfu ambapo
juhudi za kumtafuta zilianza na hatimaye kumpata Aprili 8, Mwaka huu akiwa
amekufa huku akiwa hana baadhi ya Viungo.
Mashuhuda wa tukio hilo
walisema Mwili wa Marehemu ulipatikana ukiwa pembezoni ya Mto Nkalisi uliopo
Kijijini hapo ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo kama Kichwa na Miguu ambapo
mguu mmoja ulipatikana baada ya Mbwa kukutwa akiwa ameshika na kuudondosha baada
ya kukutana na watu hali iliyowalazimu watu hao kumfutilia Mbwa huyo aliyeongoza
hadi Mwili wa Marehemu ulipokuwepo na kuwakuta Mbwa wengine wawili wakiwa
pembezoni.
Baada ya kupatikana kwa
mwili huo Taarifa ilipelekwa Polisi ambao walifika katika eneo la tukio na
kuupima kisha kuwakabidhi ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo watu wawili
walikamatwa kuhusika na tukio hilo baada ya kupigiwa kura za siri na wananchi na
kukutwa na kura nyingi ambapo wengine wanne waliachiwa kutokana na kutokuwa na
kura nyingi.
Kutokana na hali hiyo
Ofisa Mtendaji wa kata hiyo alisema mfululizo wa vitendo hivyo unatokana na
kutokuwa na Vituo vya Polisi ambapo Halmashauri ya Busokelo inakituo kimoja
kilichopo katika Mji wa Lwangwa mahali ambapo ni mbali sana kutokana na gharama
kuwa kubwa.
Kwa upande wake Diwani
wa kata hiyo Elias Mwandele alisema wananchi waache kutembea usiku ambapo
aliongeza kuwa Vilabu vya Pombe kufungwa saa mbili usiku huku akiwataka Wazazi
kutowapeleka watoto kwenye Shughuli za Machungo ambapo wameweka ulinzi wa
Sungusungu ili kudhibiti hali hiyo.
Habari picha na Mbeya
yetu
|
on Thursday, April 11, 2013
Post a Comment