Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
Warembo
waliofanikiwa kuingia Tano Bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro
wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka
kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce, Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath
Mwakitwange aliyeibuka mshindi.
Washiriki wa
shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakicheza
show ya ufunguzi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha
warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.
Mshindi wa tatu wa kinyang'anyiro hicho, Tarchisic Mtui akizungumza machache
akiwa na vazi la ubunifu lilitengenezwa kwa kutumia majani ya mti wa
Muashoki.
Mshiriki Hellen Mhando akipozi kwa picha
akiwa na vazi la ufukweni.
Redd’s Miss Higher
Learning mkoa wa Morogoro, Asnath Mwakitwange, akijinadi mbele ya majaji na
kivazi cha ufukweni
Mshiriki wa
shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Hellen Mhando
akipita jukwaani kujinadi mbele ya majaji na kivazi cha usiku.
Mkali wa muziki wa
kizazi kipya Tanzania ‘Bongo Fleva,’ Barnaba Boy akitumbuiza mashabiki wa tasnia
ya urembo wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa
Morogoro jana usiku.
KUONA PICHA ZAIDI>>>FATHER KIDEVU BLOG
Post a Comment