Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bilioni 14 zahitajika kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar


_DSC0177
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano Samia Suluhu Hassan akipata Maelezo kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Dkt Narriman Jiddawi juu ya Utunzaji wa Samaki Aquarium wakati wa Ziara ya waziri huko Zanzibar _DSC0207
 
Mhadhiri Mwandamizi wa Tasisi ya Sayansi ya Bahari ya Chua Kikuu cha Dar es Salaam Dkt NarrimanJiddawi akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan aina ya Kasa katika chumba cha Kutunzia samaki[AQUARIUM}wakati wa Ziara ya Kutembelea Tasisi za jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizopo Unguja .
…………………………………………….
Na Ali Issa Maelezo, Zanzíbar.
ZAIDI ya shilingi bilioni 14 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa chuo cha Taasisi ya Sayansi za Bahari kilichopo Buyu wilaya ya Magharibi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Hayo yamesemwa leo huko Forodhani mjini Zanzibar na Muhadhiri Dkt. Ntahondi Nyandwi wakati alipokuwa akisoma ripoti ya chuo hicho na rasilimali zake mbele ya Waziri anae shughulikia masuala ya Muungano Samia Suluhu Hassan aliyekuwa katika mfulilizo wa ziara yake kuzitembelea Taasisi za muungano hapa Zanzibar.

Amesema fedha hizo zitahitajika ili kukamilisha ujenzi wa jengo lote na miundombinu ikiwemo vifaa vya maabara, sehemu za wanafunzi wa uzamili, uzamivu, kumbi za mikutano, ofisi za programu za kimataifa, ofisi za wageni wa kimataifa na mengineyo.
Dk. Nyandwi amesema kupatikana kwa fedha hizo kutakamilisha mahitaji hayo na mengine ambapo kwa sasa ujenzi huo umefikia hatua nzuri na wameshatumia zaidi ya bilioni nne kwa kujenga miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ofisi za viongozi na madarasa.
“Kwa vile pesa za kumlipa mkandarasi hazikupatikana kwa wakati na hakukuwa na uhakika kuzipata, ujenzi ulisimama Agosti 2008 na mkandarasi aliondoka lakini kwa sasa ujenzi unaendeleo taratibu”alisema Nyandwi .
Aidha alifahamisha kuwa ujenzi huo unaendelea kidogo kidogo kadri fedha zinavyo patikana baada ya kumuomba mkanda rasi awapunguzie gharama na kuweza kumaliza mipango ya awamu ya kwanza na ya pili.
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais, Muungano Samia Suluhu Hassan amesema kuwa atamuagiza Mkuu wake wa kazi kuja Zanzíbar kujionea na yeye Jengo hilo hatua ilio fikiwa.
Aidha alisema kua ujenzi huo utaendelea kidogokidogo mpaka utapomalizika.
Maendeleo ya ujenzi wa Taasisi ya sayansi Baharini ni moja ya Taasisi za Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam kampasi ya Mwalimu Nyerere ambapo umuhimu wa Taasisi hiyo ulianza kujitokeza Mwaka 1978 chini ya sheria Na. 12 ya 1970 ya chuo kikuu cha Dar-slamu kwa tamko la Serikali Na. 34 lililo pitishwa tarehe 16 march 1979.
Chuo hicho kumalizika kwake kufanya kazi za kutafiti nyanja zote za Sayansi za Baharini, kutoa mafunzo ya uzamivu, uzamili katika sayansi ya Bahari ,kutoa ushauri wa kitalamu ,kutoa mafunzo ya Shahada ya kwaza kwa kulingsana na mahitaji ya Taifa la Tanzania kama sehemu ya Taluma kwa vitendo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top