washiriki wakijiandaa tayari kwajili ya kuanza mashindano wakiwa pamoja na Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh, Lazaro Nyalandu pamoja na waandaaji |
Mh, Lazaro Nyalandu akimtoka Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Anthony Mtaka katika mbio hizo |
mwimbaji
wa bongoflava Barnaba akiwa na Irene Kiwia manager director kutoka Frontline
Porter Novelli ambaye pia alikuwa mshiriki wa miss Tanzania wakishiri mbio hizo
ambapo walimaliza mbaka mwisho.
|
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake bi Jacquline Salum toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwatoka washiriki wenzie |
Bwana Dickson akihojiwa na wandishi wa habari baada ya kushinda mbio hizo |
Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza bwana Dicksoni Marwa. |
Dickson Marwa
alijichukulia kitita cha shillingi millioni moja za kitazanzania baada
ya kuibuka mshindi wa Tigo Ngorongoro nusu Marathon ambapo mshindi
wapili bwana Stephano Huche ambae nae ni aliweza kuondaka na kitita cha
shillingi laki tano.
mashindano haya ambayo
lengo lake ni kuhamasisha mapingano dhidi ya ugonjwa wa malaria yameandaliwa na
taasisi tanzu ya kujitolea ya kampuni ya Utalii ya ZARA Tanzania Adventures
ambayo husaidia shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujitolea na kudhaminiwa na
kampuni ya Tigo.
akizungumza na waandishi
wa habari Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema kila hatua
moja ambayo atakuwa anakimbia mkimbiaji itakuwa inahamasisha umoja katika
kupambana na malaria hatua hiyo pia ni ishara inayoonyesha nia njema ya
waandaaji wa mbio hizo kutokana na lengo la kupambana na ugonjwa huo hatari
unaoua wananchi wengi
"Kwa takwimu tulizonazo
hadi sasa ni kwamba malaria inaua watu zaidi 888,000 barani Afrika na robo tatu
wa watu hao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kwa hali hiyo, mbio
hizi zinachagiza uhamasishaji wa kupambana na ugonjwa huo"
alisema
Mbio hizo ambazo
zinafanyika kila mwaka zimeshirikisha vilabu 26 kutoka Tanzania nzima zilizo na
wanariadha 236, zilianzia katika geti la kuingilia kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro na kumalizikia katika uwanja wa Karatu mjini.
Kwa upande wa wanawake,
mwanariadha Jacquline Salum toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
aliibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano, akifuatiwa na
Zakia Mrisho aliyejinyakulia shilingi laki tatu.
akizugumza Mkurugenzi wa
Zara Tours Leila Ansell ambao ni waaandaaji wa mashindano hayo alisema
mashindano ya Mwaka huu wamepata washiriki wengi zaidi ili kuchangisha fedha kwa
ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa na Maralia pia ni kuunganisha pamoja
watalii na wananchi wa Tanzania pamoja na kukusanya fedha zitakazotumika katika
mapambano ya ugonjwa hatari wa Malaria.
Post a Comment