Mtaalam kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt.Modesta Opiya akiwanoa Waheshimiwa Wabunge katika Semina hiyo kuhusu haki za kijamii na Uchumi kwa wanawake Waheshimiwa Wabunge mbalimbali wakichangia mada iliyowasilishwa na Dkt.Modesta Opiya
……………………………………………
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa Legislative Support Project, umeandaa semina ya siku moja kwa waheshimiwa Wabunge kuhusu Haki za wanawake katika nyanza za kiuchumi, kijamii na kisiasa, kwa lengo la kuwajengesa uwezo waheshimiwa Wabunge katika maeneo hayo hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania ipo katika mchakato wa Kuandaa katiba Mpya.
Semina hii ni mwendelezo wa semina za kutoa elimu kwa waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge katika maeneo mbalimbali ya kibunge ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao ya Kibunge. Jumla ya Kamati Tano, za Kilimo, PAC, LAAC, Miundombinu, Maendeleo ya Jamii na Katiba Sheria na Utawala zimeshiriki semina hii.
Mradi huu wa Legislative Support Project, ambao upo chini ya Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) uliingia ubia na Ofisi ya Bunge mwaka 2011 kwa lengo la kujenga uwezo kwa Wabunge na Watumishi katika maswala mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Shughuli za Kibunge.
Mpaka Sasa mradi huu umekwisha toa mafunzo mbalimbali kwa wabunge ambayo yamewasaidia kuongeza uelewa wa mambo mbalimbalu katika sekta hapa nchini hivyo kuweza kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi, usimamizi wa serikali pamoja na kutunga sheria kwa ufanisi mkubwa.
Post a Comment