GAIRO,
MOROGORO, Tanzania
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi na uvunjifu
wa amani yanayoanza kushamiri bungeni na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya
hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi
waliowachagua.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa shule
ya Msingi, Gairo mkoani hapa, Aprili 18, 2013, ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
" Mambo
haya yanayofanywa na wabunge kama ilivyotokea jana (juzi), ni dhihaka
inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi waliowachagua. Baadhi ya wabunge wanafanya
vituko hivi huku wakiwa wanatambua wazi kwamba heshima waliyopewa ni kwenda
bungeni kujadili matatizo ya wananchi ambayo ni mengi kama migogoro ya ardhi.
Hili tukio la jana ni aibu ya mwaka", alisema Nape.
Alisema,
muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa kuutumia wote kwa hekima busara na
uwezo wao wote kujadili namna ya kuwezesha Watanzania kufikia maisha bora na
siyo kuutumia muda huo kujadili tofauti zao za kisiasa au namna ya kutekeleza
malengo yao binafsi ya vyama vyao.
"Hatua hii
ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha tafrani na kuvunja kanuni za bunge kwa
makusudi ni ya hatari sana, hivyo wananchi wanapswa kujifunza kwamba hawa siyo
watu wa kuwapa madaraka. Tazama hivi sasa bungeni wapo wachache sasa wananchi
wakihadaika wakawachagua na kuwa wengi bungeni patakuwaje? Hili ni fundisho
tosha". alisema Nape.
Alisema,
hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema kulijadili suala la Mkurugenzi wa
Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku wakijua
kwamba ni suala ambalo lipo mahakamani, ni la kujaribu kuingilia uhuru wa
mahakama kwa makusudi ili ifikie mahala mahakama itupilia mbali kesi hiyo kwa
kigezo cha kuinngiliwa uhuru wake.
"Haya ni
matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa na viongozi wao ikiwemo kuingilia
uhuru wa mahakama, ili hatimaye ionekane uhuru wa mahakama umengiliwa kuhusiana
na kesi hiyo na hatimaye itupiliwe mbali. Kila mwenye akili anajua kwamba huu
ni mkakati malum wa Chadema", alisema Nape
Mbali na
kulizungumzia bungeni suala ya Lwakatare, Chadema wamekuwa wakilisema pia
mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi karibu ya Mbunge wa Singida, Tuntu Lissu
kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo na kwamba mbali na
kutafuta kesi hiyo itupwe pia ni juhudi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya
mahakama.
"Inashangaza
sana, Lisu badala ya kutoa ushahidi wake mahakamani kuhusu suala hili anakwenda
kuzungumza na wandishi wa habari ili hali anafahamu wazi kwamba kesi kuhusiana
na suala hilo ipi mahakamani, tafsiri yake ni kwamba ni juhudi za Chadema
kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama au kushawishi mahakama kutupilia mbali
kesi kwa kigezo kwamna imeingiliwa uhuru wake", alisema na
kuongeza:.
"Mbowe pia
wakati akizungumza Bungeni alitumia muda mrefu kuzungumzia suala la Lwakatare
lililopo mahakamani. leo mahakama ionekane uhuru wake umeingiliwa iitupe kesi,
na hata wakati wa kuchangia bajeti ya Utumishi, upande wa Chadema badala ya
kuzungumzia sekta ya utumishi wa umma kurasa nne nzima zilihusu mambo ya
Lwakatare", huu ni mkakati mbaya sana unaolenga haki isitendeke kuhusu kesi
hiyo.
Akizungumzia
hatua ya Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutamka bungeni kwamba Mwenyekiti
wa CCM Rais Jakaya Kikwete na Chama Chake cha CCM ndiyo chanzo cha udini,
aling'aka kwamba ni kauli inayotia shaka uelewa wa mambo wa mbunge huyo



Post a Comment