DIWANI WA KATA YA MALUNGA JOHN CHAGU AKIWA
KWENYE MOJA YA MIKUTANO YAKE.
KAHAMA
Diwani
wa Kata ya Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga John Chagula, leo
amelazimika kurudisha kiwanja alichomiliki katika eneo lenye mgogoro la Igomelo
kufuatia malalamiko ya wananchi.
Hayo
yametendeka leo kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Goodluck Ole Medeye kutembelea maeneo yaliyoporwa kinyemela na kubadilishiwa matumizi mjini
Kahama.
Dhoruba
hiyo ilimkumba Chagula baada ya wananchi wa eneo hilo lililokuwa lipangwa kujengwa Soko, Kituo
cha Polisi na makanisa kudai mbele ya Ole-medeye kwamba baadhi ya viongozi hasa
madiwani wamejigawia eneo hilo huku wakijua ni la huduma za jamii.
Alipotakiwa
kujieeleza, Chagula alitamka mbele ya hadhara kwamba anarudisha mara moja
kiwanja hicho alichokijenga baada ya kuwa amepotoshwa na idara ya ardhi kwamba
ni sehemu ya makazi.
Wengine
walioagizwa kusalimisha viwanja hivyo ni pamoja na Diwani wa Kata ya Kahama
mjini Abas Omari, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mstaafu Meja Matala na Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi Kata ya Malunga Donald Igulu.
Olemedeye
amekuja Kahama kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli kwa ajili
ya kujionea migogoro ya ardhi mjini kahamaambapo amefuta viwanja vyote
vilivyotolewa kinyemela na watendaji wa idara ya ardhi wilayani humo.
kb blog
1 comments:
very gud
ReplyPost a Comment