FILAMU mpya ya
nguli wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, inayojulikana kwa jina la ‘Love
and Power’ itaanza kusambazwa kuanzia Aprili 12 mwaka huu.
Filamu hiyo
iliyozinduliwa Aprili 7 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam
ikiendana na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa nguli huyo,
tayari imeanza kuwa gumzo kubwa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa filamu hiyo, mdogo wa Kanumba, Seth Bosco, ambaye ni
msimamizi wa Kampuni ya Kanumba The Great, aliwashukuru Watanzania waliokuwa
wamejitokeza.
Alisema siku ya
juzi hawezi kuisahau katika maisha yake kutokana na kuzinduliwa kwa kazi ya
kimataifa iliyofanywa na Kanumba kabla ya kufariki dunia Aprili 7, mwaka
jana.
“Kanumba alikuwa
na ndoto za kuikomboa nchi yetu katika tasnia ya filamu, nafikiri naye Mungu
anajua ni kwanini kamchukua, hivyo yatupasa kushukuru kwa kila jambo,” alisema
Bosco.
Uzinduzi huo
ulihudhuriwa na wasanii nyota kutoka Ghana, Ama Abebrese, Ama Mc Brown na
aliyekuwa Meneja wake wa Kimataifa, Prince Richard na wasanii mbalimbali wa
filamu wa hapa nchini.
Kanumba
alifariki dunia Aprili 7, mwaka jana nyumbani kwake Sinza – Vatican jijini Dar
es Salaam, huku kifo chake kikihusishwa na msanii mwenzake, Elizabeth Michael
‘Lulu’.
Post a Comment