Hussein Bashe |
Ndg
zangu,Awali ya yote niwatakie Juma Pili Njema na Kwa Ndg zetu wanoenda kanisani
siku ya Leo waendelee kuombea Taifa letu na Viongozi wetu kufanya maamuzi ya
Busara juu ya Hatima ya Maisha ya Watanzania na Taifa kwa
Ujumla.
Nimeanza na maneno hiyo hapa juu kufatia matukio
miwili,Moja ni Tukio la Arusha na Pili ni Tukio la Maamuzi ya Baraza la Madiwani
la wilaya ya nzega.
Nzega
Halmashauri ya wilaya nzega imepitisha Bajeti na
mipango ya Mendeleo ya mwaka wa fedha 2013/4 kilichonisikitisha ni Madiwani
kujitengea milioni 82 kwa ajili ya ziara Kwenda mkoa ya Arusha ,Dodoma Kama
ziara ya kujifunza,Wakati wilaya inakabiliwa na Changamoto za uharibifu aw
miundo mbinu kufatia muda Nyingi,makazi ya wananchi wengine yameharibika,shule
za msingi na secondaries hazina Madawati,waalimu hawana nyumba ,vituo vya Afya
having dawa za kutosha,tunakabiliwa na tatiizo la Maji Mijini na
vijijini.
Wakati Hali ikiwa hivi fedha hizo ni
Intrest(RIBA) iliyotokana na fedha zilizowekwa benki Baada ya mgodi kutulipa
2bn,Wabunge wakiwa wajumbe wa kamati ya fedha wamepitisha hili,mbali hapo
wameunda tume ya Watu 15 Kwenda Dar kukutana na Katibu mkuu aw Nishati kufatilia
madai Kila mjumbe atapewa posho ya siku 80,000 kwa siku 10 mbali na posho za
madereva kwani wataondoka na gari za halmashauri,mbali na mafuta,kuna tume ya
kufatilia mji mdogo nayo inawajumbe 10 imetengewa mamilioni ya
pesa.
Mbali na Hilo wakubwa wameamua kumchukua fedha
2bn kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Nzega ikiwa na dhamira ya kutoa mikopo kwa
Wananchi aw Nzega,wanafanya maamuzi haya huku wakifahamu Halmshauri ya wilaya ya
Nzega Ina Fedha za Mfuko aw Maendeleo ya Vijana ,Mfuko aw Maendeleo ya Kina Mama
,Mabilioni ya Jk vyote hivi vimeshindwa kusimamiwa na Fedha zake kwa Miaka yote
hazijawahi kuwa na Mrejesho chanya Leo tena wanatenga fedha ili kuanzisha Benki
itakayoendeshwa na Watu wale wale,kwa Mfumo ule ule,kuwakopesha Watu wale wale
ambao Mara zote wanaposhindwa kurejesha hutumika sasa zile zile
kuwasamehe.
Huu ni mchezo kwenye maisha ya wananchi aw wilaya ya nzega ambao hawana High school ,hawana barabara za uhakika,waalimu hawana makazi,wanafunzi hawana maabara,hawana Madawati,zahanati hazina Madawa,mikopo ya Mabilioni ya Jk haikufanikiwa,mikopo ya Mfuko aw Maendeleo wa Vijana haikufanikiwa,mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Kina mama haikufanikiwa Leo zinatengwa fedha za kuanzisha Benki ya kukopesha wana nzega,kuna Mabenki mawili nzega,kuna taasisi za mikopo zaidi 5 kwa matatizo yanayokabili wilaya lie huu ni Kupoteza fedha za wananchi wa nzg kwa posho na kuandaa maradi ambayo haina Tija.
TUKIO LA ARUSHA.
Tukio la kuuwawa Kijana aw Chou cha uhasibu na
matokeo Yake badala ya kutafuta wauwaji kunatengenezwa mazingira ya kuleta
Instabillity kwa kumkamata LEMA, Kaka yangu Mulongo katika hili alivolisimamia
na kulitekeleza ameonyesha Udhaifu aw Hali ya Juu na matokeo Yake inavunjia
heshima Serekali ya Chama chetu na Kuongeza chuki dhidi ya CCM Hakukua na sababu
ya Kubahave the way he did pale chuoni,alionyesha kiburi hakua humble,hakutumia
Busara katika jambo hili.
Wakati
kuna Kijana ameuwawa,na yeye ndie Rais wa eneo lile attitude alionyesha Hakukua
na leadership pale,tunakabiliwa na uchaguzi kuna mtu ameuwawa na si Tukio la
kwanza,Nguvu iliyotumika kumkamata lema Leo CCM mkoa aw Arusha wanakabiliana na
maswali mengi kuliko Majibu,inasikitisha viongozi wanaotuwakilisha kuongoza ndio
hao tunawaona Bungeni,ndio hao Kina Mulongo na maamuzi na attitude ya kaka
Mulongo,ndio hao Kama Baraza la Madiwani aw Nzega ambao kwao semina
safari,posho,maradi isiyotekelezeka,kuunda tume ya kuchunguza madai ya
wafanyakazi ni kuitengea fungu Wakati kk Bajeti wameisha tenga fedha za kulipa
madeni halafu unaunda tume ya kuchunguza madeni ambayo umeisha
lipa.
Ndg zangu
wana CCM chuki za Watanzania dhidi ya chama chetu zinaongezeka Kila siku na hii
ni kutokana na Tabia zetu wenyewe Wakati hospitalini hakuna Vifaa vya Kina mama
kujifungulia sisi tunajitengea fedha za ziara 82m,posho za 80,000 kwa
siku,tunaanzisha miradi ambayo haitawasaidia wananchi kk kero zao za Kila
siku,Wakati mwanafunzi ameuwawa na kibaka tunatumia mabomu,Rundo la Askari
kumkamata mtu Moja kwakua si mwana CCM,wananchi nyumba zimebomolewa na
mvua,hakuna Bajeti ya kuwasaidia hawa Watu,hakuna Madawati,dawa
hospitali,tunaelekeza fedha ktk mambo yasiyogusa maisha Yao.
Unless
tubadilike na kuanza kutambua Watanzania hawajatupa madaraka ilituchezee maisha
Yao,unless tutambue uongozi ni dhamana tutendelea kuchukiwa na Leo sitashangaa
Arusha tukipoteza kata 4 zilizowazi,tunawalazimisha Watanzania kutafuta
matumaini kwa wapinzani kwa sisi wenyewe kuamua kujipa Utawala badala ya
Uongozi.Binafsi swala la nzega nimekiandikia Barua chama changu wilayan kukiomba
kutazama upya maamuzi ya Full Council na kutambua upya vipaumbele halmashauri ya
nzg inakabiliwa na Changamoto Nyingi hawatakiwi kuchezea fedha za walipa
kodi.Hili la Arusha CCM inatakiwa kutolishabikia RC amemishandle the whole
thing.
1 comments:
Bashe ni mnafiki
ReplyPost a Comment