MFANYABIASHARA,
Mkumbukwa John Shayo (37) (pichani) aliyefariki katika kifo chenye utata nchini
China amezikwa Jumatano iliyopita na kulifanya Jiji la Mwanza kutawaliwa na
majonzi.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za
mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mkumbukwa
Joseph.
Umati wa watu
ulihudhuria mazishi hayo nyumbani kwa bibi wa marehemu, Mabatini kisha kuelekea
katika Makaburi ya Buzuruga, Nyakato na kila mtu alionekana kujawa na
huzuni.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa marehemu.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa marehemu.
Watu wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
Josephat Mkumbukwa. Kushoto ni mjomba wa marehemu Erasto
Kombe.
Mkumbukwa alifariki
China na maiti yake kuhifadhiwa hospitali kwa takriban mwaka mzima na serikali
ya nchi hiyo huku mkewe, Neema Majukano pamoja na rafiki wa marehemu aitwaye
Haji Msongore wakilaumiwa kwa kushindwa kutoa taarifa mapema juu ya kifo
hicho.
Paroko wa Kanisa Katoliki Kigango cha Mabatini Nyamagana,
Charles Bundu, akiendesha ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Joseph Mkumbukwa
aliyeuwa nchini China mwaka jana.
Aidha, utata umegubika
kifo cha Mkumbukwa kufuatia rafiki huyo wa marehemu ambaye mara ya mwisho
walikwenda wote nchini Chini kudaiwa kumuoa mke wa marehemu,
Neema.
Dada wa marehemu
akisaidiwa na waombolezaji mara baada ya kuuaga mwili wa marehemu kaka
yake
Post a Comment