Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JESHI LA POLISI LATOA MAFUNZO KWA WAWAKILISHI ZANZIBAR

 
 
Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd(pichani), amelitaka Jeshi la Polisi Nchini kuongeza bidii katika kutekeleza kazi zao za msingi ili kuendelea kujenga imani kwa wananchi hatua itakayosaidia kuinua uchumi wa taifa letu.
Hayo aliyasema juzi wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja iliyowakutanisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi visiwani humo pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi walipokutana baada ya wawakilishi hao kuomba uongozi wa Jeshi la Polisi kwenda visiwani Zanzibar kuwapa elimu na kujadili juu ya hali ya Usalama hapa nchini.
Aliongeza kuwa, wananchi wanadhima na dhamana ya kulisadia Jeshi la Polisi katika kubaini na kufichua wahalifu kwa kuwa wananchi ndio wanaowajua zaidi wahalifu na wanaishi nao kuwataka wawakilishi
Akitoa Pongezi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd, baada ya kufungua semina, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema, alisema, Makamu wa Pili wa Rais amekua mstari wa mbele mara kwa mara katika kuhimiza suala la amani na utulivu ili nchi yetu iwe na ustawi imara wa kiuchumi, kijamii na kiusalama.
Akichangia mada katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Hamza, alisema, wawakilishi ni sehemu ya Polisi jamii na kuwataka wajumbe wenzake wawe wa kwanza katika kujulisha na kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu unaotokea katika majimbo yao na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema kwa kukubali kwenda visiwani humo kutoa semina ambayo itawasaidia katika msuala ya ulinzi na usalama katika majimbo yao.
Mheshimiwa Hamza aliongeza kuwa, ipo haja kwa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuendeleza Dhana ya Polisi Jamii/Ulinzi Shirikishi katika kata na Shaiha zote kwani tayari faida imeanza kupatikana.
Hata hivyo akitoa mada katika semina hiyo kuhusu maboresho ya Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Lucas Kusima, alisema moja ya maboresho hayo ni kuhakikisha ustawi wa askari unaimarishwa.
Katika kuimarisha ustawi wa askari hao Kamishina Kusima aliongeza kuwa, baadhi ya hatua ambazo zimekwisha fikiwa ni pamoja na askari kupata huduma ya matibabu kwa kutumia mfuko wa bima ya afya na upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia SACCOS ya Polisi na tayari zaidi ya shilingi bilioni 30 zimekopeshwa kwa askari.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top