MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu,
Naomi Nnko akishiriki kuimba na wanakwaya wa kikundi cha Magu One Theatre (MOT),
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani yaliyofanyika juzi
(19.4.2013) katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza.
(Picha na Emmanuel Ndege)
Baadhi ya wazee
wakazi wa Wilaya ya Magu wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Magu, baada ya kufanyiwa
upasuaji wa mtoto wa jicho ili kuwawezesha kuona tena. Kutoka kulia ni Weja
Mfalasi, Constantine Mgana na Bujingwa Ngelela.
MKUU wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana akisalimiana
na baadhi ya wazee ambao walifanyiwa upasuaji wa macho na kuwawezesha kuona tena
katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Magu, mkoani
Mwanza.
MKUU wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana (watatu
kutoka kushoto) akiwa katika Chuo Cha Ualimu Mukidoma kilichoko wilayani humo,
wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Wengine katika picha ni
viongozi na wahadhiri wa chuo hicho
MKUU wa
Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana, akiteta jambo na Mkurugenzi wa hoteli ya
Bujora Point Swimming Pool & Lodge, Benjamin Mgonzwa, baada ya ufunguzi wa
ukumbi wa kisasa wa hoteli hiyo iliyoko Kisesa, wilayani Magu katika mkoa wa
Mwanza
(HABARI MSETO BLOG)


Post a Comment