Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akiifungua Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
kuhusu uimarishaji wa Jeshi la Polisi Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Juu
wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakili
wakisikiliza Hotuba ya mgeni rasmi Balozi Seif katika semina ya Wajumbe hao
kuhusu maboresho ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa juu
wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Maafisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la polisi Tanzania
walioshiriki semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo uliofanywa na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye ukumbi wa Baraza hilo uliopo
Mbweni.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakili wakisikiliza
Hotuba ya mgeni rasmi Balozi Seif katika semina ya Wajumbe hao kuhusu maboresho
ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa juu wa Baraza hilo
uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha na Hassan Issa wa -Ofisi
ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar-Zanzibar
---
Watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini wanapaswa
kuendelea kutekeleza majukumu kwa nguvu zao zote ili kuwapa fursa Wananchi
kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku bila ya bughdha
zozote.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiifungua semina ya wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar iliyoandaliwa na jeshi la Polisi Nchini Tanzania kuhusu
maboresho ya jeshi hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Juu wa Baraza la
Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Balozi Seif alisema Jamii mara nyingi hujenga
hofu wakati inapokabiliwa na matokeo tofauti yanayohatarisha maisha na mali zao
na hii husababishwa na matendo mabaya ya ujambazi wanayokuwa wakiyashuhudia
katika baadhi ya maeneo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyatolea
mfano matukio ya hivi karibuni ya ujambazi yaliyotokea Zanzibar ambayo mbali ya
kujenga hofu kwa raia lakini pia yameitia dosari Zanzibar katika harakati zake
za kuimarisha Sekta ya Utalii.
Alifahamisha kwamba kitendo hicho kimeleta
mshituko kwa wawekezaji wa sekta hiyo ya utalii jambo ambalo linaonekana
kuhatarisha biashara ya utalii inayoweza kuporomosha mapato ya
Taifa.
Alilikumbusha Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi
kuelewa kwamba wana dhima ya kulinda maisha na mali za raia na kulitaka Jeshi
hilo kujizatiti katika kutumia mbinu za Kisayansi wakati wanapokabiliana na
wahalifu popote pale Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa
Maaskari hao kuendelea kulinda siri za raia wema wanaojilotea kutoa taarifa za
watu wanaohusika na ujambazi ili wajenge imani ya kulisaidia zaidi Jeshi
hilo.
Balozi Seif alisema Wananchi walio
wengi hivi sasa wanashindwa kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kuhofia nusalama
wao kutokana na wahalifu wanaowatolea taarifa vituoni kurejea ma majigambo
mitaani huku wakitishia usalama wa maisha
yao.
“ Wahalifu wanashikwa na kupelekwa vituoni kwa kutokana na msaada wa taarifa za Raia wema lakini baada ya saa chache unawakuta wahalifu hao wamerejea mitaani na majigambo kwa kuwatambia waliopeleka taarifa hizo kituoni. Sasa tujiulize usalama wa Raia hao wanaotoa taarifa hizo uko wapi “. Aliuliza Balozi Seif.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alilipongeza Jeshi la Polisi Zanzibar kwa hatua yake ya kuanzisha mpango maalum wa kushirikisha Jamii latika Ulinzi wa pamoja { Polisi Jamii } { Ulinzi shirikishi } ambao unaonekana kuleta mafanikio kiasi.
Balozi Seif alisema mpango huo unafaa kuendelezwa zaidi kwani zipo dalili zinazoashiria kuwepo kwa hatua kubwa ya kiulinzi ambayo inaweza kupunguza au kuondosha kabisa matukio ya uhalifu katika maeneo mbali mbali hasa zile sehemu za Vitega uchumi.
“ Tumeshuhudia ndani ya maeneo yetu tunayoishi kupunguwa kwa matukio ya wizi, unyang’anyi na hata kuwepo kwa Vijana wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kutokana na uanzishwaji wa Vikundi hivi kwenye shehia tofauti Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.
Naye akitoa shukrani zake kwa niaba ya Watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini Mkuu wa Jeshi hilo Tanzania IGP Said Mwema alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya jeshi hilo baada ya kuanzishwa mfumo mpya wa ushirikiano { Smart Partnership } ndani ya jeshi hilo.
IGP Said Mwema alisema lengo la uanzishwaji wa mfumo huo ni kuona Jeshi la Polisi Nchini linaboreka katika harakati zake za kulinda maisha na mali za wananchi hapa Nchini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/4/2013.

Post a Comment