Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho
mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo,
aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za
kuaga mwili huo zimefanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa
kwa maziko kesho.
Mmoja wa majaji akibeba
picha ya marehemu wakati majaji hao wakishuha jeneza hilo lenye mwili wa
marehemu, ili kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee
leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji ndugu wa
marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa
marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari
April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika
leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli
hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
kesho.
Mmoja wa wanafamilia
akibugujikwa machozi wakati wa shughuli hiyo ya kuaga.
Majaji wakibeba jeneza
lenye mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, wakishusha katika
gari kwa ajili ya kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee,
leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Jaji Mkuu
Kiongozi na Jaji Mkuu wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee leo kushiriki
kwenye shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo,
aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Spika wa Bunge, Anne Makinda, Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakiwa katika
shughuli hiyo ya kuaga
mwili.
Post a Comment