Mkurugenzi
wa Hoteli ya Sapphire Court ya Jijini Dar es Salaam, Abdulfatah Salim (kulia)
akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Nahodha wa timu ya wamiliki wa Magazeti
'Tando' Blogers Fc, Muhidin Sufiani, ambaye ni mmiliki wa mtanda wa
www.sufianimafoto.com, kwa ajili ya kushiriki katika Bonanza maalum la waandishi
Medi Day linalofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni kesho. Katikati
ni Meneja wa muda wa timu hiyo, Mroki Mroki. Timu hiyo ambayo inashiriki kwa
mara ya kwanza katika michezo na bonanza kama hilo, inatarajia kushiriki katika
michezo yote itakayo chezwa hiyo kesho, ikiwa ni pamoja na Soka, Netiboli,
Kukimbiza Kuku, Kukimbia na Magunia, Kuvuta Kamba, Kucheza Pool, Kuimba na
Kudansi 'Sebene' na mingineyo.
Makabidhiano yakiendelea,
hii ni Jezi ya Kipa.
Nahodha wa
timu hiyo Sufianimafoto (kushoto) akiwa na Meneja wa muda wa timu hiyo, Mroki
Mroki, wakiwa na Vifaa vilivyokabidhiwa.
Na
Mwandishi Wetu
HOTELI ya
Sapphire Court iliyopo makutano ya mitaa ya Swahili na Lindi, Dar es Salaam leo
imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya wamiliki wa magazeti tando (Blogers FC)
kwa ajili ya Bonanza la Media Day, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja
vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
Akikabidhi
vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Sapphire, hoteli iliyojizolea umaarufu mkubwa kwa
sasa nchini, Abdulfatah Salim Saleh amesema ameamua kukabidhi vifaa hivyo ili
kuunga mkono timu hiyo mpya inayoanzishwa katika tasniya ya michezo
nchini.
“Nilipopata
ombi lenu, sikutaka hata kujifikiria, nilisema nitawasadia, na huu ni mwanzo tu.
Naahidi kushirikiana nanyi zaidi na zaidi na ninawakaribisheni wakati wowote,
mimi ni shabiki wa timu yenu kuanzia
sasa,”alisema.
Kwa upande
wake, Meneja wa Muda wa Blogers FC, Mroky Mroky alisema kwamba wanashukuru kwa
msaada huo na wanaahidi kudumisha uhusiano mzuri na
Sapphire.
“Wazo hili
la kuanzisha timu ni la muda mrefu, lakini lilikuwa likisuasua, ila tukaamua kwa
vyovyote lazima tutokee kwenye Media Day ya mwaka huu. Tulipofikiria suala la
wapi tutapata vifaa vya michezo, vichwa vilituuma kidogo, lakini tunashukuru
Sapphier wametuliza maumivu hayo,”alisema Mroky.
Naye
Nahodha wa Blogers FC, Muhiddin Sufiani amesema kwamba baada ya kupata vifaa
hicyo kesho wanatarajia kuanza kuonyesha cheche zao kesho katika Bonanza la
Media Day, lengo likiwa ni kubeba ubingwa upande wa soka na kutwaa pia mataji
mengine madogo madogo.
Miongoni
mwa wachezaji nyota wanaotarajiwa kuichezea Blogers FC kesho ni Issa Michizi,
Majjid Mjengwa, Sufiani mwenyewe, Majuto Omary, Joseph Lukaza, Shaffi Dauda,
Saleh Ally, Mahmoud Zubeiry, Millard Ayo na John
Bukuku.
Bonanza la
wanahabari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), litafanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders, chini ya udhamini wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Pamoja na
wanahabari kuchuana katika michezo mbalimbali, lakini Bonanza hilo pia
litapambwa na burudani ya bendi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi
Modern.
Kutakuwa
pia na mechi maalum baina ya wanahabari ambao wameoa na wale ambao hawajaoa
utakaofanyika baada ya michezo ya kawaida baina ya vyombo vya habari
kumalizika.
Bonanza
litaanza saa tatu asubuhi kwa washiriki kucheza michezo mbalimbali ikiwemo soka,
netiboli, wavu, kuruka kichura, aina mbalimbali za riadha, kuvuta kamba na
kucheza muziki. Bonanza litamalizika saa moja usiku.
Imechotwa: Habari Mseto
Post a Comment