WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kutoa baraka kwenye tamasha la uzinduzi wa albamu ya muimbaji nyota wa nyimbo za Injili Bupe Kingu ijulikanayo iitwayo‘Andika Ndoto Yako’.
Uzinduzi huo unaotarajia kuiteka Dar utafanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Kanisa la Oasis kwa Mchungaji Ntepa nyuma ya Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Akizungumza kuhusiana na uzinduzi huo Dar es Salaam jana, Bupe alisema maandalizi yamekamilika na Waziri Chikawe amethibitisha atakuwepo siku hiyo. Mbali na Chikawe Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu ni baadhi ya miongozi waalikwa wanaotarajia kuwepo siku hiyo.
“Nataka kutoa shukrani za dhati kwa Waziri Chikawe kwa Moyo wa ukarimu alioonesha wa kukubali kuja kutoa baraka katika uzinduzi wa albamu yangu ya kwanza pamoja na majukumu mengi aliyonayo hasa kipindi hiki ambacho Bunge linakaribia kuanza,” alisema.
Katika uzinduzi huo ambao utaanza saa nane mchana hakuna kiingilia na hivyo amewataka wakazi wa jiji kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya aina yake.
Wanamuziki watakao msindikiza kwenye uzinduzi huo ni Martha Mwaipaja, Stella Joel, Mchungaji Deborah Ntepa, Faraja Ntaboba, Mwanamapinduzi, Janet Mlema, Flora Kaguo na wengine wengi.
Albamu ya ‘Andika Ndoto Yako’ inabeba nyimbo saba ikiwepo iliyobeba albamu.
Nyimbo nyingine kwenye albamu hiyo ambayo inapatikana kwenye VCD, DVD na audio CD ni pamoja na ‘Mwanadamu’ , ‘Upendo Wa Mungu’, ‘Jambo Gani’, ‘Bathimayo’ , ‘Usifadhaike’ na ‘Asante’.
“Dhumuni langu la kutoa albamu hii ni kueneza Injili kwa njia ya uimbaji, kama kuna faida yoyote itapatikana kuhusiana na kazi hii, hiyo itakuwa ni bonsi kwangu na nategemea kutumia kununua vifaa vipya vya muziki kwa sababu vya sasa vingi vimechakaa,” alisema.
Bupe ni Mke wa Mtume Moses Kingu wa Huduma ya Uzima Katika Neno inayopatikana Mbezi Malamba Mawili jijini ambapo katika moja ya nyimbo zake sauti ya Kingu imesikika.
credits: Fullshangwe
Post a Comment