Na Fadhili Athumani, Monduli
DICKSON Marwa kutoka katika kambi ya Holili, mkoani kilimanjaro kwa mara nyingine tena ameonesha umwamba katika mchezo wa riadha baada ya kuibuka mshindi katika mbio za kilometa 10 za Sokoine Marathon 2013, kwa kutumia muda wa dakika 30:42:43.
Dickson alishinda mbio hizo ikiwa ni takribani wiki moja tu tangu ashinde mbio za ngorongoro Marathon zilizofanyika mjini karatu, na kuwazidi wanariadha John Leornard wa W.spirit aliyetumia muda wa
dakika 30:44:92 na Msenduki mohammed wa Hakika ya Arusha aliyetumia muda dakika 30:50:05.
Kwa upande wa mbio za wanawake kilometa 10, Catherine Lange wa magereza ya Arusha aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dakika 38:17:56, huku akimuacha kwa mbali mshindi wa pili, Fadhila Salum wa
JWTZ, aliyemaliza mbio hizo kwa muda wa dakika 38:51:75.
Nafasi ya tatu ilienda kwa Selina Amos, aliyetumia muda wa dakika 39:10:15 huku nafasi za nne na tano zikienda kwa Florah Yudah (41:46:06) na Rosalia Fabiano (41:49:04), wote kutoka JWTZ ya Arusha.
Kwa kuibuka washindi, Dickson Marwa na Cartherine Lange walizawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja huku washindi wa pili wakiondoka na shilingi elfu themanini na wa tatu nao wakiondoka na shilingi elfu
sitini na cheti kila mmoja.
Mbio za Sokoine Marathon, ambazo zilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu za kifo cha Edward Moringe Sokoine aliyefariki, Aprili 12 mwaka 1984, zimefanyikia katika kata ya Monduli Juu, Wilayani Monduli, mkaoni Arusha na kushirikisha wanariadha zaidi ya 500.
Sokoine Marathon zilihusisha mbio za umbali wa kilometa 2 kukimbia na kutembea kwa watoto na watu wazima VIP na zile za kilometa kilometa 10 kwa wanariadha wazoefu. Viongozi waliohudhuria Mbio hizo ni pamoja na Waziri wa Michezo, dk Mukangala, Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, Mbunge wa Viti Maalum, Namelok Sokoine, Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema pamoja na viongozi wengine akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Dickson Marwa Akimaliza mbio hizo |

Lange akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo |
Marwa katika mahojiano na waandishi wa habari mbalimbali |

Post a Comment