Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
Mechi tano kati ya
sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja
(live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa
hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.
Msemaji wa TFF,
Boniface Wambura
Kwa mujibu wa
Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max
Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na
matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van)
yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.
Mechi hizo ni kati ya
Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT
Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini
Tanga.
"Tatizo hilo pia
limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii.
SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya,"
alisema.
Tshunungwa amekutana
na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa
kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week
kabla ya ligi kumalizika msimu huu.
Post a Comment