Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la
Misikiti Tanzania (BAMITA),Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango
kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya
Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo
jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti
Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa kukabidhi
msaada wa sh. mil 5 kwa Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzana,katika
makabidhiano yaliyofanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania
(BAMITA),Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung'he waliofika ofisini
kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya
kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza
maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum
Sung'he akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akitoa
shukrani zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya
kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza
maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo
yamefanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti
wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum
Sung'he akikabidhi kwa Mh. Lowassa barua ya shukrani kutoka Baraza la Misikiti
Tanzania (BAMITA).Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania
(BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Post a Comment