Mh. Namelok Moringe Sokoine akikabidhiwa cheti cha
kushiriki mbio za Edward Moringe Sokoine Mini Marathon na mkuu wa mkoa wa Arusha
mh. Magesa Mlongo jana wilayani Monduli Arusha.
Namelok
Sokoine ni binti wa hayati Moringe Sokoine ambaye ni mfano wa kuigwa na wanawake
wote nchini kwa kusimama kidete katika maandalizi ya kumbu kumbu za baba yake,
aliyefariki mnamo tarehe 12/4/1984 kwa ajali ya gari wakati huo akiwa ndiye
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania.
Dada huyu ni mchapa kazi, anapenda watu wote bila kujali cheo au kitu chochote alichonacho. Namelok Sokoine amewashukuru viongozi na watu wote waliohudhulia siku ya kumbu kumbu ya hayati waziri mkuu Edward Moringe sokoine na kutoa ahadi ya kuwakaribineni pia kwa mwakakesho kushiriki tukio hilo kwani watakuwa wakiazimisha miaka 30 tokea hayati Edward Sokoine afariki dunia. Mgeni rasmi atakuwa Mh. rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na pia kutakuwa na mbio za kilomita 42. |
Post a Comment