Kitendo cha wabunge sita wa CHADEMA kufukuzwa juzi bungeni limezidi
kuchukua sura mpya hapa nchini.
Wapo
wanaodai kuwa adhabu hiyo haikuzingatia kanuni za bunge na badala
yake ilitolewa kwa jazba za Naibu spika wa bunge.
Mbali
na hao, lipo kundi linaloamini kuwa adhabu hiyo ni sahihi na wanadai
kuwa ni ndogo na pengine ingekuwa vyema kama ingeongezwa ili liwe
fundisho kwa wabunge wengine
Kwenye kipindi cha tuongee asubuhi Star TV ,mhadhiri
mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Dr Bana,
amesikika akisema kuwa adhabu waliopewa akina Lissu ya siku tano haitoshi na
walitakiwa wapewe adhabu hata ya miezi mitatu na wakatwe mishahara pia.


Post a Comment